NGUVU ZA KUZIWIA MBINU ZA SHETANI
Ni muhimu wakati tujaribu kuelewa Shetani na njia zake tukifuata mwongozo wa Bwana wetu. Tunahitaji kujua jinsi adui anajaribu kuzuia jitihada za Mungu kati yetu.
Chuki cha Shetani kwa wafuasi wa Kristo ni halisi sana. Anadharau kila kitu ambacho Mungu anasimamia, na atafanya yote anayoweza ili kuzuia watu inje ya ukweli. Nimeona hasira yake tangu nilikuwa mtoto mdogo huko Puerto Rico. Wazazi wangu walikuwa wanajulikana katika kanda kwa ajili ya mazoezi yao ya uchawi, kwa hiyo nilikua nikiona nguvu Shetani anazo juu ya wale walio chini ya ushawishi wake. Wakati mama yangu aligeuka kuwa Mkristo, ilikuwa pigo kubwa kwa kazi ya Shetani aliojenga ndani ya familia yangu. Alikuwa mmoja wa washirika wake wakubwa, na sasa alikuwa amegeuka adui yake mkali.
Baada ya mama yangu kutoa uzima wake kwa Yesu, mke wangu, Gloria, na mimi tulimtembelea nyumbani kwake. Kila usiku wakati tulipokuwa huko, saa tatu kamili ya subuhi, Gloria alikuwa anaamushwa na sauti ya kutisha nje ya dirisha lake. Alipotuambia kuhusu hilo, mama yangu akacheka na akasema, "Usiruhusu hilo likusumbue. Tangu nimegeuka kuwa Mkristo, mapepo wamekasirika nami. Waambie wanyamanze, kisha urejee usingizi."
Gloria hakuwa na hakika ya kufikiria ushauri wake kwa sababu hakuwahi kuona mambo ambayo familia yangu iliowahi kupitia. Lakini ndivyo nilivyojaribu kukabiliana na Shetani na mapepo yake yenye maalifa. Licha ya mashambulizi yao, wakijifanya kuogopewa, njia bora ni kuelekea tu kwa nguvu za Yesu. Yote Shetani anajaribu kufanya ni kujenga upepo katika maisha yetu kutuzuia kuwaambia watu kuhusu Yesu.
Mtume Paulo alitukumbusha kwamba Yesu "amezivua enzi na mamlaka" na "kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo" (Wakolosai 2:15). Kupitia tendo hili, Yesu alitoa kwa kila mmoja wa wafuasi wake uwezo wa kuondoa uovu wakati wowote unapojitokeza mbele yetu.
Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka ( Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).