NI NINI KINACHOZUIA KAZI YA MUNGU NDANI YETU?
"Basi nitasifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili nguvu za Kristo ziwe juu yangu" (2 Wakorintho 12:9). Mtume Paulo alikua dhaifu kwa sababu ya shida na dhiki lakini wakati alipotiwa chini, hakukata tamaa. Alifurahi katika mchakato wa kuwa dhaifu kwa sababu ilikuwa ni siri ya nguvu zake na Kristo, na kutokana na udhaifu huo akawa na nguvu.
Baadhi wanaweza kuwa na kazi isiyokamilika, ugonjwa, hali ya upweke sana au talaka. Mambo hayo ni sababu nzuri za kukata tamaa lakini jambo moja ambalo linazuia kazi ya Mungu katika maisha yetu ni uenyewe tu. Wakati Yesu alisema tunapaswa kuchukua msalaba wake na kumfuata, alikuwa anatuomba sisi kujikataa wenyewe (tazama Luka 9:23). Kiburi chetu kinasema, "Ninaweza kufanya hivyo mimi mwenyewe." Lakini Yesu anasema, "Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, yeye akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huzaa matunda mengi; kwa maana pasipo mimi humwezi kufanya chochote" (Yohana 15:5).
Yesu anaangalia ulimwengu huu, iliojazwa na watoto waliochanganyikiwa wanaendelea kwenda kwa kujaribu kueka haki yao wenyewe, wakijaribu kumpendeza kwa njia yao wenyewe, na anaita misalaba. Msalaba unamaanisha kutuvunja na kutotesha jitihada zote za kibinadamu. Hawezi kuzibiti yote mpaka tunajikana na kumlilia, "Baba, siwezi kwenda kwenye hatua nyingine! Nguvu zangu zimeisha! Nisaidie!"
Wapenzi, usifikiri kwamba kesi yako ni hukumu kutoka kwa Mungu na usijihukumu mwenyewe. Kwa kweli, unachotumia ni ushahidi wa upendo wake kwako, huku kukuletea ushindi mkubwa na ukomavu. Wewe uko katika shule yenyewe ya ufwasi wa Kristo, basi shangilia kuwa kama unapofaulu na kumtii, utapata nguvu zake zenye kushinda zaidi!