NI WAKATI GANI UTAAMINI YALE MUNGU ALIOHIDI?

David Wilkerson (1931-2011)

Unajua Wakristo ambao hulalamika daima juu ya jinsi wanavyojisikia kutosha? Wao daima wanajidharau na kujilinganisha na wale wanaowapendeza, wakifikiri, "Mimi si kitu kama yeye. Haina matumaini kwangu."

Unaweza kukumbuka hadithi ya Agano la Kale ya wapelelezi wa Waisraeli waliotumwa kutathmini Nchi ya Ahadi. Wakarudi wakisema, "Naam, ni nchi yenye wingi maziwa na asali, lakini pia imejaa watu wenye nguvu nyingi na miji mikubwa yenye kuwa na kuta ndefu. Hatuwezi kupanda mulima ili twende tupigane  dhidi ya watu hawa. Ikilinganishwa nao, sisi tuko kama nyasi tu"(tazama Hesabu 13).

Sasa, hawa watu hawakuhukumu Mungu. Hawakusema kamwe, "Mungu hawezi. Yeye hana nguvu ya kutosha." Waliogopa kusikia kutoamini kama hiyo, lakini badala yake walijikuta wenyewe, wakisema," Sisi ni kama mende mdogo machoni pa adui zetu."

Hiyo siyo unyenyekevu na sio hatia, majadiliano wasio na hatia. Badala yake, ni chukizo kwa Mmoja ambaye ni nuru ya ulimwengu. Nuru hii inatuamuru tuamini, "Nayaweza mambo yote kupitia Kristo mwenye kunipa nguvu" (Wafilipi 4:13).

Unaona, unapolalamika kwa kutoweza na udhaifu wako, hujisikia chini, unamtupa Bwana wako. Vipi? Kwa sababu unakataa kuamini au kutembea katika Neno lake. Wapelelezi wa Waisraeli waliangalia sana udhaifu wao wakuwa tayari kuacha, lakini majibu ya Mungu yalikuwa nini kwa hofu zao na kutokuamini? "Bwana akamwambia Musa, Je! watu hawa watanidharau hadi lini'? Wataniamini hadi lini? Najapokuwa nimefanya ishara kati yao? "(Hesabu 14:11). Mungu aliwaagiza kwa dhambi moja: kutokuamini.

Leo Bwana anawauliza watu wake swali lile lile aliloliuliza Israeli: "Lini mutakapoamini kile nilichowaahidi? Nilisema nguvu zangu zingekuja wakati wako wa udhaifu. Hamupaswi kutegemea nguvu za mwili wenu. Mimi ni Yehova, nguvu za milele, nami nitawafanya muwe na nguvu kupitia nguvu zangu."