NJIA YA KUELEKEA UTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu Kristo, Mwokozi wetu, anasimama peke yake katika utakatifu kamili. Kwa sababu Yesu peke yake ni mtakatifu na mkamilifu, Mungu hamtambui mtu mwingine yeyote. Kwa hiyo, ikiwa tutapokewa daima na Baba wa mbinguni, lazima tuwe ndani ya Kristo, kwa neema tu ya Kristo na kwa kupitia sifa isiyofaa kwetu wenyewe.

"Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwanjia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba." (Waefeso 2:16). "Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sharia ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani" (2:15).

Kwa sababu ya kazi ya Kristo msalabani, mtu hakuweza kujaribu tena kuwa mtakatifu kwa kuzingatia sheria ya Mungu. Hakuweza kuwa mtakatifu kwa kazi nzuri, vitendo vya haki au jitihada yoyote ya kibinadamu. Badala yake, Baba alipendelea kukubali mtu mmoja tu kama mtakatifu: mtu mpya, aliyefufuliwa.

Wakati mtu huyu mpya alipomwonyesha Baba yake wote wanaomwamini, Baba alijibu: "Niwapokea kama watakatifu, kwa sababu wako ndani ya Mwana wangu mtakatifu" (tazama Waefeso 1:6).

Tunajumuisha mwili wa mtakatifu huu, asiye na hatia. "Basi nyinyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake yake" (1 Wakorintho 12:27). Tumefanywa mfupa wa mfupa wa Kristo na mwili wa mwili wake na tunachukuliwa katika familia yake: "Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake" (Waroma 12:5).

Kwa sababu sisi tuko ndani ya Kristo, tumefanywa kuwa watakatifu. "Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote" (Warumi 11:16). "Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi" (Yohana 15:5).

Njia ya Kuelekea utakatifu sio kupitia uwezo wa binadamu, bali kupitia imani katika Bwana wetu Yesu Kristo. Nini jibu la ajabu kwa kilio cha wasiwasi wa watu wengi ambao wana kiu ya kuwa watakatifu. Sisi ni watakatifu kama tunapumzika katika utakatifu wa Kristo! Utakatifu wetu ni utakatifu wake - unaozunguka kwetu, matawi, kutoka kwenye mizizi.