ROHO INAENDELEZA KAZI KUWA HAI

Gary Wilkerson

"Petro, mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale wateule wa Utawanyiko  wakaao hali ya ugeni katika  Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithynia, kama vile Mungu Baba, alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na: Neema na amani ziongezwe kwenu.

"Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi ilituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lililo lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo kutoka kwa wafu; tupate na uruthi usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya Imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho" (1 Petro 1:2-5).

Petro alikuwa na msisimko wa kuwasiliana na makanisa ya miji ambayo alipitia ikisafiri. Walikuwa wakimbizi, baada ya kulazimishwa kutoka nje ya nchi yao, lakini Petro alikuwa anaonyesha picha nzuri kwa ajili yao. Roho yake ilikuwa yenye kusisimuwa kama alivyosema kwamba alikuwa akitakaswa kwa Roho, ya kumtii Yesu, na ujuzi wa Baba. Alikuwa akisema jinsi Mungu angevyowaweka na kuwapa urithi katika Mwokozi ambaye angefunuliwa "wakati wa mwisho." Wangelizaliwa tena kwa tumaini lililo hai katika Yesu.

Utakaso huwawezesha waamini kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa kuwa mtiifu; anaendeleza kazi hiyo kuwa hai. Unaweza kumfanya ashindwe wakati mwingine, lakini ikiwa umekoshwa na damu ya Yesu, nguvu zake bado zinafanya kazi ndani yako, hivyo usitembee ndani ya hukumu na aibu.

Kama vile hawa "wateule waliokuwa ukimbizini" kwa kuwa walihamishwa kutoka makazi yao, na wewe unaweza kukabiliana na mambo katika maisha yako ambayo yanaonekana kuwa mabadiliko na vikwazo, lakini unaweza kuwa na uhakika kwamba kila wakati Mungu anasema hapana, ni kwa sababu anaandaa kitu bora zaidi, kitu ambacho kitakuweka mahali ambapo utafikia malengo ambayo amekuwekea. Yeye ni hai na anafanya kazi - na ahadi zake ni kwa ajili yako!