SALA ZA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Sala ni siri ya ukuaji wa kiroho, lakini ikiwa tunakwenda kwa kiti cha enzi tu kwa ajili ya kuimarisha na mahitaji yetu binafsi, tunakuwa na ubinafsi. Biblia inatuonyesha kwamba hatuwezi kuacha kuomba sana kwa mahitaji ya wale walio karibu nasi na kutupa mifano ya "sala zenye manufaa" (angalia 2 Wakorintho 1:11).

Watu mara nyingi wanasema, "Nitawaombea," na wanaweza kuomba mara moja au mara mbili na kisha haraka kusahau mahitaji ya mtu mwingine. Sala la musaidizi wa kweli ni mtu anayeomba kwa urahisi kuhusu mahitaji ya wengine. Hawaombei kwa mara moja tu kisha kuacha kuomba. Hapana, yeye huombea siku baada ya siku.

Sala zako hazihitaji kuwa ndefu. Tu, sema ombi lako na uamini Mungu atakusikia.

Hii ilionyeshwa kwangu wakati mmoja nilipokuwa nimelala kitandani. Mmoja wa wajukuu wangu alikuja na kusema, "Baba, naenda ku kuombea." Msaidizi wangu mdogo akaweka mkono wake juu ya kichwa changu na akasali, "Yesu, mufanye kuwa bora zaidi mahari pote."

Nilitabasamu na kumshukuru kwa kuomba. Lakini aliendelea kunitazama. Hatimaye, akasema, "Wewe umepona. Simama!" Kwa hiyo niliamka - na niliponywa. Sala yake ya imani imenisimamisha kwenye miguu yangu.

Uokoaji mkubwa unafanyika wakati watakatifu wa Mungu wanamtafuta kwa bidii na imani kama ya watoto kwa mahitaji ya wengine. Tunaweza kuangalia Maandiko na kuona jinsi Mungu anatembea kwa nguvu kama matokeo ya sala na ujasiri kuwa waisaidizi katika sala. Angalia jinsi Paulo anatoa ushuhuda wa kusisimua wa hili:

"Naamu sisi wenyewe turikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijiyumainie nafsi zetu, bali tumutumaini Mungu, awafufuaye wafu, aliye tuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; amabaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa; ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu. " (2 Wakorintho 1:9-11).