SAUTI ZENYE KUSHITAKI

Gary Wilkerson

Wakati mwingine mimi huamka katikati ya usiku nikiwa na wasiwasi unaozunguka bure. "Mshtaki wa wa ndugu" ananongoneza, "Wewe sio mzuri; huna maana, uko mzigo kwa wengine. Angalia historia yako, ni mara ngapi umeshutumu." Shetani anapenda kuwatesa Wakristo lakini wakati Yesu alipokuja, alisema. "Hilo linaisha sasa!" Kisha anaongeza mushangao wa kuhakikisha: "Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba" (Yohana 5:45).

Kama watu wa Mungu, wakati mwingine tunaweza kujihukumu wenyewe. Paulo anasema, "Hao waionesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao . . . na mawazo yao yenyewe kwa yenyewe akiwashitaki . . . wao" (Warumi 2:15). Je, ni nani Paulo anayesema hapa? Ni Mkristo ambaye anajaribu kuishi nje ya vituo vya Agano la Kale kwa kujitahidi kumpendeza Mungu peke yake. Mkristo huyu anajiambia mwenyewe, "Nimefanya vizuri kwa Bwana kila wiki, hivyo hakuna sababu siwezi kuweka pamoja wiki nyingine kama hii."

Wengine wanaweza kutushtaki, kama ilivyotokea katika kesi ya mwanamke mzinzi, wakati viongozi wa kidini walimleta kwa Yesu na wakamuomba amshtaki pia. Lakini Yesu alijibuje washitaki wake - na wawakili wake? "Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe" (Yohana 8:7). Yesu akageuza uangalifu ambapo ulikuwa: kwa dhambi zao wenyewe. Na wakaondoka mmoja mmoja (tazama 8:9).

Sauti inaweza kupiga kelele katika masikio yetu lakini wakati zikifanya, tutasikia sauti nyingine juu izo zote: "Kondoo wangu waisikia sauti Yangu; nami nawajua, nao wanifuata" (Yohana 10:27).

Kuwa bado na kusikia sauti ya Roho Mtakatifu akisema, "Yesu amekuweka huru." Naomba Mungu akusaidie kujenga juu ya msingi imara unaozingatia upendo wa utukufu wa Yesu - na kufurahia katika neema yake ya ajabu!