SHIKAMANA NA MUNGU

Gary Wilkerson

Wafuasi wa Yesu walikusanyika pamoja kwenye Chumba cha Juu wakati Roho Mtakatifu alipokuja na kujaza kila mtu mahali hapo (tazama Matendo 2:1-4). Umati wa watu ukiwa umekusanyika nje, Petro alishikwa moyo na Roho kuhubiri na watu elfu tatu walikuja kwa Kristo (ona Matendo 2:41).

Kufuatia uamsho huu wa kihistoria wa kiroho, Petro na Yohana walikuwa wakitembea kuelekea Hekaluni walipokutana na mwombaji aliye kilema. Wakati mtu huyo akiomba msaada, Petro akamwambia, "Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini kile nilicho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama, utembee” (Matendo 3:6). Mara moja mtu huyo mwombaji alipona.

Muujiza huu ulikuwa na athari ya kusisimua: "Wakati alipokuwa akiambatana na Petro na Yohana, watu wote wakakusanyika sana, wakakimbia pamoja nao kwenye ukumbi wa nyumba" (3:11). Mtu huyo aliyeponywa 'alishikamana na Petro na Yohana; ilikuwa kana kwamba alikuwa akisema, "Uwepo wa Mungu ni kweli. Nimekuwa hapa kwa miaka, naomba msaada, lakini sikuwahi kuona kitu kama hiki. Mungu ameichochea roho yangu kuliko kitu chochote ambacho nimewahi kujua."

Mungu anapenda kushikamana. Yeye anapenda moyo unaomfuata na kulia, "Bwana, utukufu wako ni mkubwa sana kuupitisha. Nashikilia tumaini unalonipa - tumaini la uponyaji, mabadiliko, kwa uwepo wako katika maisha yangu na ulimwengu wangu."

Katika msitali wa 11, watu wote walishangaa na wakaja kuona yaliyotokea. Wakati Mungu anajidhihirisha utukufu wake, ukuu wa nguvu yake unahitaji umakini wa kila mtu karibu. Ikiwa muujiza kama huo ungefanyika kanisani kwako, hakutakuwa na nafasi ya kutosha kushughulikia makutano ambayo yangekuja kutazama na kuwa sehemu yake. Unaona, watu wana njaa ya kuguswa na Mungu maishani mwao, waumini na wasio waamini. Kila mtu anataka uzoefu mpya wa maisha, kitu ambacho ni halisi.

Mungu ameweka ukuu wake wote, utukufu na nguvu katika chanzo kimoja: Kristo. Kwa sababu ya nguvu yake ya kubadilisha, unaweza kuona uwepo wake na kuishi maisha ya ushindi ambayo hutoa ushuhuda kwa wote wanaokuzunguka.