SIRI YENYE MAISHA YA KUSHINDA

David Wilkerson (1931-2011)

"Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya ya imani yenu iliyo takatifu sana,na kuomba katika roho Mtakatifu. Jilindeni katika upendo wa Mungu,huku mkingojea rehema ya Bwana wetuYesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.” (Yuda 20-21).

Nilipokuwa nikiisoma aya hizi katika Yuda, nikasikia Roho akisema kwa sauti ya utulivu: "Daudi, nataka uingize ukamilifu, na furaha ya upendo wangu. Una haki ya teolojia, lakini bado haujazoea ma pumuziko ya kweli unatokana na kujiweka menyewe katika upendo wangu. Hadi sasa, umekuwa tu ndani yake kutoka juu hadi kwenye miguu yako. Kuna bahari kubwa kwako ili uogeleye ndani yake.“

Biblia imejaa ukweli wa upendo wa Mungu. Hata hivyo ninakubali kwamba wakati mwingine mimi hujiacha kujiuliza jinsi Bwana aliweza kunipenda. Siyo kwamba nina shaka kwa upendo wake. Ni kushindwa zaidi kwa upande wangu kujiweka katika ujuzi na uhakika wa upendo wake kwangu.

Ufunuo wa upendo wa Mungu huja kwa sehemu tunapozaliwa tena. Ikiwa ungewauliza Wakristo wengi kile wanachojua kuhusu upendo wa Mungu kwao, wangejibu, "Najua Mungu ananipenda kwa sababu alimpa Mwanawe afe kwa ajili yangu.” Wangeweza kunukuu Yohana 3:16,” Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa Mwanawe pekee,ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele.”

Ni wakati mzuri sana wakati unafahamu ukweli huu: "Mungu alinipenda wakati nilikua nimepotea, sikufanya, nilikua mgeni. Na alithibitisha upendo wake kwangu kwa kutoa dhabihu ya Mwanawe kwa niaba yangu.”

Kuelewa upendo wa Mungu ni siri yenye maisha ya ushindi. Watu wengi sana huwa baridi kwa kiroho kwa sababu hawajui upendo wa Mungu kwao. Hawajui silaha yao kuu dhidi ya kukabiliana na Shetani, ni kuwa na hakika kabisa juu ya upendo wake, ambao huja kupitia ufunuo wa Roho Mtakatifu.