SUBIRI ROHO MTAKATIFU

Jim Cymbala

Nimegundu kwamba waumini wengi hawana mabadiliko ya asilimia tano kutoka kwa kile walichoamini wakati walikuwa na miaka miwili tu katika Bwana. Tunakabiliwa na mistari ya Biblia na ukweli usiostahili kwetu, tunajificha nyuma, "Lakini hii ndiyo njia ambayo tumefanya kila wakati. Hii ndio tuliyoamini kila wakati."

Tunaposhika Biblia na tusipo omba msaada wa Roho Mtakatifu, ni kama kusema, "Mungu, fanya jambo jipya ndani yangu, lakini sitaki kubadilisha chochote ninachoamini." Hilo ni sala lisiyo la kawaida, Je! Sio ivo? Haishangazi sisi kukua kidogo sana katika imani yetu na kuona watu wachache sana waongofu kwa Kristo.

Mara nyingi, tunapata ufafanuzi wetu kwa mambo muhimu ambacho sio kile Roho anatuonyesha katika Maandiko, lakini kwa kile tulichoona kinakua ndani ya kanisa. "Oh, hiyo ni ibada inapaswa kufanana, kwa sababu ndiyo njia hio hio tulivyofanya kila kanisa nililohudhuria." Ni vigumu kwa sisi sote kuja kwa Neno la Mungu na kusema, "Roho Mtakatifu, nifundishe, hata kama inakwenda kinyume na kile ambacho nimekuwa na hali ya kuamini." Na kwa uhakika tunapaswa.

Inachukua muda kwa Roho Mtakatifu kutufundisha maana ya kifungu. Ikiwa hatuwezi kumngoja Roho Mtakatifu, kumwamini, tunaweza kukua tuna baridi na kuanguka nje ya ushirika wakuwa na Mungu hata wakati tunapokuwa na ibada kila siku.

Mtume Paulo aliandika, "'Mambo amabayo jicho halikuaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu' - Mambo amabayo Mungu aliwaandalia wampendao -  Lakini haya nimambo Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu" (1 Wakorintho 2:9-10, msisitizo aliongeza).

Kila wakati tunapofungua Biblia, hebu acha tusimamishe na kuomba, kama ni sekunde kumi na tano au dakika kumi na tano, kwakuomba Roho kutufundisha. "Unifundishe akili na maarifa, Maa nimeyaamini maagizo yako" (Zaburi 119:66). Kisha maisha yetu yatafanana kama ya Yesu kila siku.

Jim Cymbala alianza Hema la Brooklyn (Brooklyn Tabernacle) akiwa na wanachama wasio zidi  ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.