THAMANI YA MAWAZO YA MUNGU

Gary Wilkerson

Jambo muhimu zaidi naweza kukuambia ni kwamba Baba yako wa mbinguni anakupenda! Ni ukweli rahisi kwamba nina hakika umesikia mara nyingi, lakini Wakristo wengi wana shida kuelewa. Hata hivyo, ikiwa unataka kuwa na mafanikiyo kwa Yesu, kweli huu mwamba mugumu lazima uwe katikati.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda, nitamutuma yeye kwenu" (Yohana 16:7). Kwa kweli, Msemaji ni Roho Mtakatifu, Msaidizi wetu, Mfariji wetu.

Kuishi katika dunia hii iliyovunjika, imesababisha shida kwa njia yetu na baadhi yake inaweza kuwa ya kushangaza, inayohusisha afya yetu, watoto wetu, maisha yetu. Ili tupate yote, tunahitaji kuwa na ufahamu wa upendo wa Baba yetu, kwa sababu hiyo ni kweli Roho Mtakatifu ataleta kukumbuka wakati wa maumivu makubwa kupitia majaribu.

Daudi alionekana akijua uwepo wa Msaidizi wakati aliandika, "Maana mawazo yako ni ya thamani nyingi kwangu, Ee Mungu! Hayawezi kuhesabiwa" (Zaburi 139:17). Tafsiri nyingine inasema, "Je, ni mawazo ya thamani gani kwangu kwako unajishughulisha juu ya hayo."

Kutambua kwamba Mungu anafikiri juu yetu ni la kushangaza. Ni jambo moja kujua kwamba Bwana anatupenda; hiyo ni ukweli tu wa kitheolojia. Lakini ni lingine kujua kwamba yeye anafikiri kila wakati juu yetu - kwamba, kwa kweli, yeye kamwe hataacha kufikiri juu yetu. Hata hivyo Mungu anatuambia kupitia Zaburi ya Daudi, "Wewe huhitaji kujitahidi ili kupata mimi kukusikiliza. Mimi tayari nimekwisha angazia juu yako."

Daudi anasema kwamba mawazo ya Mungu kuhusu wewe ni ya thamani. Niyenye upendo kwa njia ambayo huwezi kamwe kufahamu kikamilifu. Wewe ni mpendwa kwa Baba yako wa mbinguni na anapenda kampuni yako - na mipango anayo kwa ajili yako ni daima kwa faida yako.