UCHUNGUZI WANDANI KUTOKA KWA UVUMILIVU WA YOBU

David Wilkerson (1931-2011)

Mjadala wowote juu ya mateso na majaribio lazima uanze na mwamini mwenye kukata tamaa wakati wote - mtumishi mwenye haki, mwaminifu, mwenye kuogopa Mungu, kujitolea kwa sala na ibada. Hata hivyo, wakati huzuni na shida zilipokuwa zimeharibisha maisha yake, huyo mtu alianza kunungunika sana kuhusu Mungu wakati wa mateso yake. "Kama ningemwita naye akaniitikia; hata hivyo singeamini kuwa amesikiya sauti yangu. Yeye anipondaye kwa dhoruba, na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu" (Yobu 9:16-17).

Yobu alipoteza kila kitu alichompenda: familia yake, afya yake, mali yake, hata tumaini lake. Taarifa juu ya Mungu katika kifungu hiki hapo juu ni moja tu ya wengi ya mtu maskini huu kwa maumivu yake alivyoongezeka.

Taifa letu linaingiya haraka ndani ya kipindi cha shida, wakati ulimwengu haujawahi kuona kama huu. Hata sasa, waumini wengi waliojitolea wanakabiliwa na shida ambazo uzoefu wao wa awali haukuwaandaliwa kwa hayo. Wakristo wanaona ndoa zao zinajaribiwa; wengine afya zao zimeshuka; wengine wana shida ya kifedha; na vijana wanapotea katika ukicha wa saa.

Katika siku zijazo, hatuwezi kuruhusu matumaini yetu ya kupumzika katika bomba la ndoto fulani, kwakuamini kwamba Wakristo watakuwa na kinga kutokana na mateso. Hata hivyo, tunaweza kuhakikishiwa kuwa Baba yetu wa mbinguni atakuwa mwaminifu kututunza kupitia shida zetu zote na kutuokoa, kama alivyofanyia Yobu.

"Mmesikia habari ya subira Yobu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma" (Yakobo 5:11).

Yobu alivumilia na Mungu akamrudisha yote aliyopoteza na zaidi. Vivyo hivyo, unapokuja kupitia jaribio lako, utakuwa na uaminifu wa moyo wa kweli kwamba Mungu ana udhibiti wa maisha yako. Kisha utakuwa na uwezo wa kushuhudia wema wa Mungu, kama vile Yobu alivyofanya aliposema kwa ujasiri, "Ingawa ananiua, bado nitamtumaini" (Ayubu 13:15).