UHURU WA UTUKUFU KWA KUTOKA KWENYE HOFU

David Wilkerson (1931-2011)

Hali katika dunia leo husababisha hofu kuongezeka. Tunashuhudia maneno ya Yesu yanatokea: "Na katika dhiki ya mataifa wakishangaa ... watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakaoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika" (Luka 21:25-26). Kristo anatuonya, "Bila tumaini ndani yangu, umati wa watu utaenda kufa kwa ajili ya hofu."

Kwa wafuasi wa Yesu, hata hivyo, wale ambao wanaamini ahadi za Mungu za kulinda watoto wake, kuna uhuru wa utukufu kutoka kwa hofu zote. Kwa kweli, wote wanaokuja chini ya utawala wa Kristo, hawana haja ya hofu tena ikiwa watashikilia siri ifuatayo: Uhuru wa kweli kutoka kwa hofu ni kujitoa kabisa kwa maisha ya mtu mikononi mwa Bwana.

Kujitoa wenyewe katika utunzaji wa Mungu ni tendo la imani. Ina maana kujitia kabisa chini ya nguvu zake, hekima na huruma, imesababishwa na kuhifadhiwa kulingana na mapenzi yake pekee. Ikiwa tunafanya jambo hilo, Mungu wa ulimwengu anaahidi kuwa mwenyeji wa kwetu kabisa - kulisha, kuvaa na kutukinga, na kulinda mioyo yetu na uovu wote.

Yesu alitoa mfano wa mwisho wa aina hii ya kujitowa kutakatifu wakati alipokuwa msalabani. Kabla ya kutowa pumuzi yake ya mwisho, alilia kwa sauti, "Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu" (Luka 23:46). Kristo aliweka uwangalifu wa maisha yake yote na siku zake za badae milele na milele katika ulinzi wa Baba. Na kwa kufanya hivyo, aliweka nafsi za kila kondoo wake ndani ya mikono ya Baba.

Unaweza kujiuliza, "Je, Yesu hakusema kuwa alikuwa na nguvu zote za kuweka maisha yak echini na kuyachukua tena?" (Tazama Yohana 10:18). Kwa kuwa alikuwa na uwezo wa "kuchukua tena maisha yake," kwa nini alijiuzulu katika mikono ya Mungu ili ihifadhiwe? Jibu ni rahisi: Yesu alifanya hivyo ili kuweka mfano wa imani kwa kondoo wake wote waifuate.