UJASIRI NA UHAKIKA KWA SIKU NGUMU

Carter Conlon

Ninaleta habari njema! Milele sio tu pekee tunayotarajia. Ninaamini mioyo yetu itajazwa na furaha kubwa hata katikati ya siku ngumu (angalia Yohana 16:33). Kutakuwa na ushirika katika Mwili wa Yesu Kristo kama wewe na mimi hatukuwahi kupitia uzoefu katika maisha yetu.

Kutakuwa na furaha tunapokusanyika pamoja - nyakati zakawaida ambapo hatutaki kuondoka nyumba ya Mungu. Kweli Bwana atakuwa nguvu zetu na wimbo wetu. Naye atatupa fursa ya kumtukuza kwa kuruhusu wengine kuona nguvu Zake ndani yetu wakati wa mateso. Watenda dhambi watakuja kwetu na kusema, "Tuambie sababu munaendelea kuwa na matumaini!" Unaona, tutaweza kuwa na matumaini kwa sababu tuliisikia onyo la Mungu na kuchukua wakati wa kujiandaa.

Haijalishi mambo magumu huwa yanaweza kuja, kwa hakika sioni Kanisa la Yesu Kristo likiondoka katika mshtuko. Ninaona kanisa lenye kushinda - Kanisa ambalo linaheshimu Kristo, amesimama kwa ujasiri katika nguvu za Roho Mtakatifu, kama alivyoanza katika kitabu cha Matendo.

Katika wakati huu wa maandalizi, sala yangu imekuwa, "Bwana, chukua kila kitu nje ya maisha yangu ambayo italeta udhaifu ndani ya moyo wangu. Hebu achia Roho wako ndani yangu anipe nguvu na uafanye maisha yangu kukuletea heshima. "Ninakuhimiza kumwuliza Bwana mambo ambayo unahitaji pia. Mwombe ushujaa, uvumilivu, na ujasiri (ona Wafilipi 1:20-21). Mwombe neema ya kutoacha katika jaribio lako la sasa au kwa wale wanaokuja.

Ninawahakikishia, Mungu hatakuacha! Na si tu wakati wa mateso lakini kupitia hao yote milele na milee, huwezi kamwe kujuta baada ya kuweka ujasiri wako ndani yake.

Carter Conlon alijiunga na wafugaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji aliyeanzisha, David Wilkerson, na akachaguliwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.