"UKO WAPI?"

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo ambao wanashindwa kuomba hawatambui hatari waliyo nayo. Unaweza kusema, "Basi ni nini ikiwa Wakristo wengine hawaombi? Wao bado wanaamini - watasamehewa na kwenda mbinguni."

Baba yetu wa mbinguni anafahamu kama tunaishi wakati washuguli nyingi, na mahitaji mengi juu ya wakati na nguvu zetu, na Wakristo wamejipata katika shughuli na kazi nyingi kama mtu mwingine yeyote. Hata hivyo, siwezi kuamini Mungu kama anachukua sana ukataaji wetu kwakutomufikilia, ambayo ilimugalimu Mwana wake peke maisha yake.

Iliumiza Baba kumtuma Yesu ili adhihakiwe na kusulubiwa ili tuweze kumwendea kwa uhuru. Lakini siku baada ya siku hupita na wengi wa watoto wake hawamkaribie mpaka wakati wanapohudhuria kanisa Jumapili. Wakati Adamu alijificha kutoka kwa Bwana katika bustani ya Edeni, Mungu akamwuliza, "Uko wapi?" (Mwanzo 3:9). Bila shaka, Mungu alijua mahali amabo Adamu alikuwa, lakini alikuwa anauliza kwa kweli Adamu kwa nini alikuwa amekataa kuwa na ushirika naye.

Wakristo ambao wanashindwa kufikia upatikanaji wao kwa Baba huishia katika hali kama ile ya kanisa la Sardi. Bwana alimwambia Yohana, "Na kwa malaika wa kanisa lilioko Sardi andika ... 'Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, lakini umekufa'" (Ufunuo 3:1). Yesu anasema, "Unaweza kuwa mtu mzuri anafanya kitu chochote kwa mtu yeyote, lakini kipengele cha kifo kinaingia ndani ya maisha yako kwa sababu ya kutojali kwako. Kitu kimoja cha ulimwengu kimekuchafuwa."

Je, ni uchafu unaojulikana hapa? Ukosefu wa sala! Waumini wa Sardi hawakuwa makini katika sala, wakisubiri Bwana na kumtafuta kama walivyokuwa awali. Walikuwa wanyonge lakini Bwana anawaambia katika Ufunuo 3:4: "Wachache wenu wanastahili na hwataki kupoteza uwepo wangu."

Haraka sasa, nenda kwenye chumba cha siri cha maombi. Amekupa kumufikia na anaahidi kukutana na mahitaji yako yote.