UKWELI, WA MAISHA MENGI

Gary Wilkerson

Wakati Roho inatufanya tuongeye kwa upendo, tunapaswa kufanya hivyo. Hivi karibuni wakati tulikua tunakula chakula cha mchana na mke wangu, nilihisi nia ya kumwambia mmoja wa watumishi wa mugahawa katika eneo letu kwamba Yesu alimpenda. Hakuwa na jibu lakini baadaye nikamwona akiwaambia wafanyakazi wengine kile nilichosema, ambacho hatukutalajia kukiona. Kisha jambo la kushangaza lilifanyika. Tulipokuwa tukiondoka, mhudumu tofauti alinisimamisha na kuwuliza kama ningependa kuomba pamoja naye!

Huyo ni mfano wa tofauti kati ya dini na upendo wa Yesu. Kupenda Yesu kunamaanisha kuhubiri ushuhuda hata wakati inaweza kukufanya uonekane kuwa wazimu - kisha utaona nguvu za Mungu zikitembea.

Wengine wanafikiri kuwa Mkristo unahitaji kujua sheria za kiroho au kuomba sala fulani. Lakini sivyo Yesu alivyoelezea imani kwa Nikodemo, Myahudi mwenye ujuzi wa dini. Nikodemo alikuwa na wakati mgumu kuelewa kile Yesu alimaanisha kwa kuwa "kuzaliwa mala ya pili." "Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?" (Yohana 3:4).

Nikodemo alikuwa anajaribu kuelewa njia za Mungu kupitia akili zake, lakini Yesu alisema kuwa njia za Mungu hazijafanyika kwa njia ya mwili wetu: "Amin, amin, nakwambia, Mtu isipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Kilicho zaliwa na mwili ni mwili; na kilicho zaliwa kwa Roho ni roho" (3:5-6).

Rafiki, tumepewa kitu bora kuliko dini. Ni wakati wa kuinuka na kufuata Kristo kwa upana. Moyo wa kile Yakobo anachoita "Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu" (Yakobo 1:27, msisitizo wangu) ni kuchukua upendo tuliyoujua na kuugawana kwa uhuru na wengine. Inatowa hofu yoyote juu ya kile tunachopaswa "kumfanyia Bwana," na kuiludilisha na moyo wa kupokea na kutoa upendo wake. Huyo ni ukweli, wa maisha mengi!