"UMENIJUA"

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana anatuuliza, "Je, Unaamini kweli kama ninaona magumu unayopitia sasa hivi?"

Labda unaposoma ujumbe huu, unakwenda kupitia kitu ambacho kinamwomba afanye kazi kwa niaba yako. Hali ya tatizo lako inahitaji jibu.

Je, unaamini Mungu kama anachunguza kila hatua yako, jinsi baba anavyofanya na mtoto wake wachanga? Je, Unaamini yeye yuko katika kazi kama Baba yako mwenye upendo, mwenye kujali - akinyunyizia machozi yote, kusikia kila mulio, akitembea juu yako?

Hiyo ndiyo njia kamili ambayo Biblia inamuelezea. "Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki na masikio yake hukielekea kilio chao ... Walilia, naye BWANA akasikia akawaponya na taabu zao zote” (Zaburi 34:15, 17).

"Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao" (Zaburi 103:13).

Neno la Kiebrania kwa huruma hapa linamaanisha "kukumbatiya, upendo, kuwa na huruma." Maandiko yanasema Mungu anakumbatiya mikononi mwake wale wote wanamuogopa (kumwamini). Na yeye anakuaambia, "Najua mawazo yako yote, wasiwasi zako zote. Najua kila vita unapaswa kukabiliana nao na ninashughulikia kwa mambo yote."

Daudi aliandika kifungu kinachojulikana kuhusu suala hili: "Ee BWANA, ume ... na kunijua. Wewe wajuwa kuketi kwangu na kuondoka kwangu;umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umupepeta kwenda kwangu nakulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote. Maana hamna neno ulimini usilolijiua kabisa, BWANA” (Zaburi 139:1-4).

"Maana mawazo yako ni ya thamani gani kwangu, Ee Mungu, ni kiasi kikubwa chao! Ikiwa ningezihesabu, wangekuwa zaidi kuliko mchanga" (139:17-18).

Daudi anasema, "Mungu anajua yote juu yangu, anaona kila hoja yangu na mwenendo wangu, hata mawazo yangu, popote ninapogeuka, yupo pale."