UMEVUNJIKA MOYO, LAKINI BADO MUNGU ANAENDELEA KUKUPENDA

David Wilkerson (1931-2011)

Kwa mimi, mmoja wa watu wenye kunivutia zaidi katika Agano la Kale ni Yakobo, mtudanganyifu, mfunga kiwani. Lakini Mungu alimpenda mtu huyu sana.

Yakobo alikuwa amemudanganya ndugu yake pacha Esau kutokana na haki yake ya kuzaliwa na kuiba baraka kutoka kwa baba yake, Isaka - baraka iliyokuwa ya Esau. Esau alipojua yale Yakobo aliyoyafanya, aliamua kumwua ndugu yake na akaweka vita vingi kati yao. Lakini licha ya hilo, Bwana alimleta Yakobo kuwa baraka ya agano la babu yake, Ibrahimu, na baba yake, Isaka (angalia Mwanzo 28:14). Halafu Mungu aliongeza baraka hizi za ajabu: "Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, name nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliokuambia" (28:15).

Kwa kweli Mungu alimwambia, "Sitakuacha kamwe, Jacob, na huwezi kamwe kufanya musukumo ambao sishiriki ndani. Madhumuni yangu yatatimizwa kwako, bila kujali mambo unaopitia!"

Ni ahadi gani! Ni vigumu kwangu kupata imani, wema au neema yoyote ndani ya Yakobo, kwa hivyo angewezaje kuwa baba wa agano la kusudi la milele la Mungu? Kweli, napenda kumwuliza Bwana, "Uliona nini ndani ya mtu huyu? Wewe ni mtakatifu na mwenye haki, na hutazama kwa aina ya vitu alivyofanya. Kwa nini hawukumulekebesha badala ya kumbariki baada ya kuiba na kudanganya?

"Mungu aliona kitu ndani ya moyo wa Yakobo ambayo ilitoa upendo wake mkubwa na hamu ya kumbariki. Tunasoma, "Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja nay eye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea" (Isaya 57:15), na Mungu alijua kwamba Yakobo alikuwa na roho ya kutubu, iliyovunjika.

Tumesikia kwamba wanadamu wanaangalia yalio nje tu, lakini Mungu daima anaangalia moyo. Alijua kuwa kitu kiko ndani ya moyo wa Yakobo kilikuwa kinatamani kugeuzwa.

 Na ndivyo hivo Mungu anatuangalia ndani yetu!