UNATAKA KUTUMIWA NA MUNGU?​

Carter Conlon

Hizi ni nyakati ambapo mtu, au labda watu wengi, wanafahamu nia ya Mungu ya kurejesha na kuponya. Wanaelewa nia yake ya kutuchukua, si kwa nguvu zetu, bali katika udhaifu wetu. Baada ya yote, Maandiko haituambie kuja kwenye kiti cha enzi cha Mungu wakati tunapokuwa na nguvu; badala, tunakuja wakati sisi ni dhaifu. "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" (Waebrania 4:16).

Wakati wa kuamka kiroho hutokea wakati watu wanaanza kusikia Bwana akizungumza: "Najua wachungaji wenu wamewaongoza watu wao ndani ya uzaifu, kwa kuunda mfumo wa kidini ulio wa zunguka ili uwasaidie kuimalisha makosa yao. Na najua watu wamefanya dhambi na wamesahau njia zangu, lakini bado naendelea kuwa na shauku, mara moja zaidi, kuwa na mwenye huruma."

Mungu anaita wanaume na wanawake kwa kutaka kutumia utukufu wake. Kumbuka, hayitakiwe kuchukua wingi wa watu ili kubadilisha taifa. Hayitakiwe kuchukua watu mia kubadilisha eneo lako - inachukua mtu mmoja tu ambaye anaamini kwamba Mungu ni tayari kuonyesha huruma. Hata hivyo, ikiwa hakuna mtu anayesonga mbele, watu ambao wangeweza kuhurumiwa, watapotea.

Ikiwa unataka kutumiwa na Mungu katika saa hii, lazima uwe na shauku ya kusonga mbele katika imani. "Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao" (Waebrania 11:6).

Tumaini Mungu kwa uwezo wa kukamilisha yote aliyokuitia kufanya. Ingawa unaweza kujisikia kama uko na kitu kidogo chakutoa, leta icho unacho na kuamini kwamba atakichukua na kubadilisha kizazi chako. "Nilimtafuta mtu!" (Angalia Ezekieli 22:30) - Mungu yuko anamtafuta yule atakayekuja kwa ujasiri na kuwa sauti ambayo inasema huruma ya Mungu.

Carter Conlon alijiunga na wafugaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji aliyeanzisha Kanisa hilo, David Wilkerson, na akachaguliwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.