UPIMAJI: KUZUNGUKWA NA MAADUI

David Wilkerson (1931-2011)

Petro anaandika: "Bwana anajua jinsi ya kumkomboa mtu kutoka kwa majaribu" (2 Petro 2:9). Na mahali pengine, mtume Paulo anaandika: "Hakuna jaribu lililowapata nyinyi, isipokuwa yale ambayo ni ya kawaida kwa mwanadamu; lakini Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe zaidi ya uwezo weno, lakini pamoja na majaribu pia atafanya njia ya kutorokea, ili mweze kustahimili” (1 Wakorintho 10:13).

Ni wazi kuwa Mungu hataki kutuweka katika majaribu yetu. Yeye hapati utukufu wowote kutoka kwa kujaribiwa kwa watoto wake - lakini kutoka kwa matokeo ya majaribio yetu! Kuna njia moja tu ya kutoroka majaribu yetu na hiyo ni kwa kupitisha mtihani. Fikiria juu yake. Ulipokuwa shuleni, hatimaye “ulitorokaje”? Ulipita mitihani ya mwisho - na ikiwa haukupita, ulirudishwa darasani.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli ya zamani, wakati Mungu aliwaleta kwenye Bahari Nyekundu. Mungu alikuwa akijaribu watu wake, akiwajaribu, akiwathibitisha. Aliwaleta ukingoni mwa uharibifu, akawazunguka na milima pande mbili, bahari mbele yao na adui aliyewakaribia kutokea nyuma (soma hadithi hiyo katika Kutoka 14).

Maneno ya Yakobo, "wakati mnapoangukia katika majaribu mbalimbali" (Yakobo 1:2), inarejelea majaribio ya Israeli. Kifungu hicho kinamaanisha, "kushushwa ndani ya shimo na kuzungukwa na maadui." Hii ndio ilifanyika na Israeli - Mungu aliwatupa katika hali ngumu ya kibinadamu. Alitaka watu wake watambue kutokuwa na msaada na kusema, "Tunakumbuka jinsi Mungu alivyookoa kutoka kwa mapigo na malaika wa kifo. Mungu alituokoa wakati huo na atafanya tena! Tufurahie uaminifu wake."

Unaweza kujiuliza ni kwa jinsi gani Mungu angeweza kutarajia Israeli kuwa na majibu ya aina hiyo; baada ya yote, walikuwa binadamu tu. Lakini Mungu anataka kitu kutoka kwa sisi sote katika nyakati zetu za shida kubwa. Anataka tumpe dhabihu ya shukrani.

Yakobo aligundua siri hii wakati alipotowa mashauri, "Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu" (Yakobo 1:2). Alikuwa akisema, "Usiache! Tengeneza madhabahu moyoni mwako na kutoa sadaka ya kushukuru katikati ya majaribu yako.” Jinsi unavyojibu katika shida huamua matembezi yako na Mungu baadaye. Kwa hivyo leta kwake sadaka yako ya shukrani!