USALAMA WETU KAMA WATOTO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alimwita Roho Mtakatifu "Msaidizi." "Rakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, yeye ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliowaambia" (Yohana 14:26, KJV). Ni jambo moja kumjua Roho Mtakatifu kama Msaidizi wetu, lakini pia tunapaswa kujua jinsi anatufariji ili tuweze kutofautisha faraja gani ya mwili na yale ya Roho.

Njia ya Roho ya kumfariji imeelezewa waziwazi katika Maandiko. Haijalishi shida, jaribio, au mahitaji, huduma yake ya faraja imekamilika kwa kupitia kuleta ukweli: "Naye atawapa Msaidizi mwingine ... ndiye Roho wa kweli" (Yohana 14:16-17).

Ukweli ni kwamba, faraja yetu hutoka kwa kile tunachojua, sio tunachohisi. Ukweli pekee huzidi hisia, na huduma ya faraja ya Roho Mtakatifu huanza na ukweli huu wa msingi: Mungu hakuchukiye wewe. Anakupenda! "Na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumimininwa katika mioyo yetu ya Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi" (Warumi 5:5). Neno la Kiyunani hapa lina nguvu zaidi kuliko tafsiri inavyoonyesha. Inasema kwamba upendo wa Mungu unasababishwa na "Kujazwa hapo na hapo zaidi" ndani ya mioyo yetu na Roho Mtakatifu.

Adui anaweza kuja kama mafuriko, kuleta hofu, hatia au mkazo, lakini tunaweza kusema ombi hili mara moja: “Roho Mtakatifu, ni hudumie mimi, ni fundishe, na unikumbushe ahadi za Yesu kuhusu usalama wangu kama mtoto wa Mungu."

"Hakuna jaribio lililowazidia ninyi, isipokuwa lililo kawaida kwa kila mwanadamu; ila Mungu ni maminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya mlango wa kutokea, ili mweze kustamili" (1 Wakorintho 10:13). Paulo anasema kwamba munapigana vita sawa na vile ambavyo wa walipitia watakatifu wa Mungu duniani kote. Jaribio lako silo la kipekee au linalokuhusu wewe tu. Haijalishi nini unayoendelea kupitia, Roho Mtakatifu huja na ukweli unaoleta faraja.