USIOGOPE WAKATI MBINGUNI INAONEKANA KIMYA
Nyuma yakusulubiwa na kuzikwa kwa Yesu, wakati huo Petro na wanafunzi wengine waliamua kukutana pamoja. Walikusanyikia nyuma ya mlango iliofungwa, wakiofia maisha yao, waliposikia maneno haya ya kusisimua: "Yeye yu hai!"
Hapo ghafla, Yesu alitembea kupitia mlango uliofungwa katika mwili wake aliyefufuliwa na akawaambia, "Amani iwe pamoja nanyi" (Yohana 20:19). Alikuwa akisema, "Usiogope! Mimi ndimi, Bwana wenu. "Sasa, niambie, kama ungekuwa katika chumba hicho, je, ungeweza kusema hili kwamba ulikuwa mtazamo mkubwa wa ajabu hujawahi kushuhudia? Je! Ungeweza kuwa na hakika kwamba hutakuwa na mashaka tena kamwe?
Kwa kweli, ni nini kitu kikubwa Zaidi kilichofuatia kuhusu mambo ya kiroho yote? "Petro akawaambia," Naenda kuvua" (Yohana 21:3). Wale sita kati ya wanafunzi walimfuata Petro kuelekea ziwani, kwa kweli wakarudi katika maisha yao kama wavuvi. Kwa nini? Nini kilichotokea kwa huduma kubwa Mungu aliowaitia?
Watu hawa walianguka katika huzuni kubwa kwa sababu ya kitu ambacho Yesu alikuwa amewaonya kuhusu: "Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni ... ninyi mtahuzunishwa" (Yohana 16:19-20). Kristo alijua kwamba wafuasi wake wa kujitolea wangepitia kipindi cha chini sana baada ya kurudi mbinguni; Walikuwa wakisumbuliwa na ukosefu wake wa kimwili katika maisha yao. Hata ingawa alikuwa ameahidi kuwa pamoja nao (tazama Mathayo 28:20), ilionekana kuwa alikuwa akiwaacha ili wafanya hivyo peke yao.
Je! Ulishawahi kupitia na msemo kavu wakati ulipohisi kama Mungu amekuacha peke yako? Huenda umekuwa ukiisikia sauti ya Mungu wazi na ushirika wako pamoja naye ulikuwa wa ajabu. Kisha siku moja uliamka na mbingu zilionekana kama chuma shaba.
Wapendwa, wakati hii itatokea, usiogope! Petro anatushauri, "Msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu ... lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini" (1 Petro 4:12-13). Ukweli ni kwamba, ingawa hauwezi kuonekana kama hivyo, ikiwa uko kwenye ardhi kavu, uko kwenye njia yako ya vitu vingi katika kutembea kwako kwa kiroho.