UTAJIRI WA AJABU WA NEEMA YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Maandiko yanasema, "Lakini kwake  ninyi mmepta kuwa katika Kristo Yesu, ambaye alifanywa kwetu kuwa hekima itokayo kwa Mungu, na haki na utakaso na ukombozi" (1 Wakorintho 1:30). Usitowe kwa maneno yote katika aya hii. Kwa ufupi, lengo la injili ni ukombozi na neema ya Mungu inajumuisha kila kitu alichotufanyia kupitia Kristo kwa kutukomboa kutoka kwa nguvu za shetani na kutuleta katika ufalme wa nuru yake tukufu!

Uadilifu (ambayo ni kuhesabiwa haki) ni msingi wa neema. Ili kuhesabiwa haki na Mungu inamaanisha kusamehewa dhambi zote na hatia na kuchukuliwa kuwa mtakatifu na mwenye haki mbele zake. Je! Ulipataje msamaha na kukubalika mbele za Mungu? Je! Ni kwa sababu Mungu aliona kitu kizuri kwako, haki ya asili ambayo ilimvutia kwako? Ulipata kibali chake kwa kutii na kuwa na wema?

Hapana - sivyo! Neno linasema, "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, na sio kutoka kwenu; ni zawadi ya Mungu, wala sio kwa matendo, asije mtu akajisifu.” (Waefeso 2:8-9).

Hakuna mtu huwa mtakatifu au mwadilifu kwa kazi zake mwenyewe, utii au uaminifu. Badala yake, mambo haya yote ni matokeo ya imani katika nguvu ya damu ya Kristo kutufanya tukaribishwe mbele za Mungu.

"Bali kwa imani ya Kristo Yesu, sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa Imani yay a Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili itakayohesabiwa haki” (Wagalatia 2:16). Kufanywa haki na imani ni jambo gumu sana kwa mwili kulikubali. Tunataka kupata wokovu wetu lakini lazima tunyenyekeye kwa haki ya Kristo na tukubali wokovu wake. Hiyo ndiyo njia ya kukamilisha uhuru.