UWE NA MOYO MKUNJUFU

Gary Wilkerson

"Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji" (Mithali 16:32).

Je, sio kuvutia? Tunataka kutoa maisha yetu kwa Injili na kwenye uwanja wa umisiyonari, lakini isipokuwa sisi kukomaa na kukua na kulisha moyo wetu na nafsi zetu, kisha kuchukua mji utakuwa tu - kuchukua mji. Na kutakuwa na mji uliojaa wasiwasi, wenye kuchanganyikiwa, wenye kukata tamaa na watu wenye shida.

Kuchukua mji kwa ajili ya ufalme wa Mungu kwa kweli kunamaanisha kuwa na moyo kamili sana na furaha vya Bwana kwamba tunahamia kwenye mwelekeo ujao. Kwa hiyo hii ina maana lazima tuwe na moyo wetu wenyewe, angalia na udhibiti "mji wetu wenyewe."

"Lindamoyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima" (Methali 4:23).

Je, Unaona kile kinachosemwa hapa? Mambo yote ya maisha kutoka moyoni. Wengi wetu kama waumini wanajitahidi kupata vitu hivi lakini tayari vilisha tolewa kwetu katika Kristo Yesu.

Petro anasema kwamba Yesu "ametupatia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa" (2 Petro 1:3).

Tunafundisha kwamba Agano Jipya la msalaba wa Yesu Kristo ni kazi ya kumaliza. Amani na furaha yote atakayekupa tayari umekwisha kupewa.

Unapokuwa na maumivu na unakabiliwa na huzuni na kukata tamaa, unasema kwamba hutaki kuhisi mambo haya. Lakini unapofunga sehemu mbaya za moyo wako, sehemu za maumivu, pia hufunga sehemu nzuri.

Kwa hiyo linda moyo wako kwa kua mukunjufu na uombe Roho Mtakatifu kukusaidia kukabiliana na maumivu katika maisha yako. Usijifiche kutokana na hayo. Chunga shamba lako la mizabibu – na kushughulikia maswala. Lakini kumbuka, yote haya inachukua muda, hivyo usiwe mukosa subira wakati unaruhusu Roho Mtakatifu kufanya kazi yake.