UZIMA WENYE KUJAA

Gary Wilkerson

"Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya” (Mithali 13:17).

Mjumbe mwaminifu huleta nini? Mjumbe mwaminifu huleta afya!

Mtu anawezaje kuleta afya? Je, Mtu asiye na afya huleta afya? Je, Moyo uliojeruhiwa au mtu ambaye hajashughulika na hali yake ya moyo huleta uponyaji kwa wengine? Namna gani kuhusu mtu anayepigana na hisia zisizo za kudhibiti? Je, Aina hiyo ya mishonari huleta injili nzuri kwa nchi ya kigeni? Kwa mji kama ule unayoishi?

Tunaposema, "Sisi ni wamisionari ..." hamu yangu ni kwamba sisi ni wamisionari wenye afya. Kwamba tutaleta afya; nikwamba tutakuwa wajumbe waaminifu.

Hebu fikiria kile tunachoenda kuwa waaminifu. Ndio, kuleta injili kwa ulimwengu unatuzunguka, ndio, kuleta msaada kwa wale wanamahitaji. Lakini jambo la kwanza ambalo lazima tuamini zaidi ni hali ya moyo wetu wenyewe. Lazima tuwe na moyo wenye nguvu na wenye afya mbele ya Bwana.

Je, hauwezi kutamani sana hilo, rafiki yangu? Je, hauwezi kutamani tu kuponywa na kutakaswa, na kuwa na ustawi wa kiroho wenye nguvu ndani? Je, unataka ungeamka asubuhi na uwe na uzima na furaha na amani na wingi ambavyo Yesu ameahidi?

Alisema, "Nimekuja kuwapa uhai na uhai wa kiroho ili muweze kuishi maisha mabaya na kuishi maisha yakuumiza. … na yahasira. ... na wasiwasi.” Subiri! Je, ndivyo Yesu alivyosema? Au alisema, "Mimi nilikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10)?

Uzima wenye kujaa! Afya! Kamili! Nguvu zayidi! Nguvu! Mwenye ujasiri! Tunapaswa kujitahidi kuwa Wakristo ambao wanatambua kuwa nguvu hii hutoka katika moyo ambao umeponywa, iko inafanywa kuwa yenye afya, na yote ndani yake, na ndani yake pekee.