VITA VYA SHETANI DHIDI YA KANISA

David Wilkerson (1931-2011)

Kitabu cha Ufunuo kinatuambia kwamba katika siku za mwisho, Shetani atafufuka kwa ghadhabu na kupigana vita "na mabaki." Bila shaka, mabaki hayo ni Mwili wa Kristo, unaohusishwa na wote "wanaozingatia amri za Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo" (Ufunuo 12:17).

Sisi katika kanisa la Kristo tunaongea mara nyingi juu ya mapambano ya kiroho; Vita vinavyoelezewa katika Ufunuo ni mashambulizi ya duniani kote amabayo Shetani ameanzisha dhidi ya Mwili wa Kristo: "Alipewa nafasi ya kupigana na watakatifu" (13:7).

Kila mwamini anajiunga katika jeshi kubwa la Bwana, na Shetani anafanya vita vya pepo dhidi ya jeshi hili. Mtume Paulo anasema kwamba kila upande wa vita, "Hatufanyi vita kwa ajinsi ya mwili; maana silaha za vita yetu si za kimwili" (2 Wakorintho 10:3-4).

Kuna "maeneo ya vita" mengi duniani kote. Katika Amerika, vita vya Shetani dhidi ya kanisa ni ongezeko la mafuriko ya kudumu ya kujifurahisha kwa kila kitu na kujivunia vitu. Silaha zake katika vita hivi ni upendo wa pesa na ulevyi wa kujifurahisha. Lakini kuna uwanja mwingine wa vita katika vita hivi: vita binafsi vya kila mmoja ya watoto wa Mungu.

Kila muumini duniani anakabiliwa na vita vyake binafsi. Biblia inasema, "Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu ... wakati wa vita, na wakati wa amani" (Mhubiri 3:1, 8). Hivi sasa unaweza kufurahia wakati wa amani. Ninamshukuru Mungu kwa majira kama hayo katika maisha, wakati furaha inatokea. Wakati wako wa vita utapokuja, inawezekana kuhusisha mapambano yanayojuwa wewe mwenyewe pamoja na Mungu.

Sisi wote tunajua hadithi ya Mfalme Daudi, mtu mwenye haki ambaye alimtumikia Mungu kwa uaminifu, lakini akaanguka katika dhambi ya uzinzi. Daudi akageuka kwa machozi yenye uchungu na akalilia Mungu akiwa na uchungu; unaweza kusoma kuungama kwake katika Zaburi ya 38 na hasa katika Zaburi ya 69. Aligundua kuwa neema ya Mungu ya kweli ilikuwa ya kutosha na akasema, "Avikomesha vita" (Zaburi 46:9).

Katika kila mgogoro wa kibinafsi unayokabiliana nao, endelea kuweka macho yako na mawazo yako juu ya hili: huruma na upendo mzuri wa Mungu haviwezi kushindwa kamwe.