VITA ZAIDI YA VITA VYOTE

David Wilkerson (1931-2011)

"Vita vimetokea mbinguni" (Ufunuo 12:7).

Tunasikia majadiliano mengi leo kuhusu vita - vita dhidi ya ugaidi, vita katika Mashariki ya Kati, vitisho vya nyuklia kutoka mataifa mbalimbali. Hakuna katika historia paliwahi kuwa wakati wa vita kama huu duniani kote. Na kwa sababu ya mawasiliano ya haraka tunayo sasa, karibu mara moja tunapokea ripoti za mabomu, za kutekwa, na idadi kubwa ya vifo.

Ninaamini kwamba Yesu alisema juu ya haya: "Mtasikia habari za vita na uvumi wa vita" (Mathayo 24:6). Na kama vile Kristo alivyotabiri, mioyo ya watu inawashinda kwa ajili ya hofu: "Watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu" (Luka 21:26). Vita tunavyoona vinasababisha hofu ulimwenguni, lakini vita hivi ni dalili za vita kubwa zaidi. Unaona, kuna kweli vita moja tu vinavyoendelea na hivi vita-zaidi ya-vita vyote inafanyika mbinguni - vita kati ya Mungu na ibilisi.

Vita hii ilitangazwa kutoka muda wa miaka mingi iliyopita. Ufunuo inatuambia, "Mikaeli na malaika wake wakapigana na yule joka [Shetani]; yule joka akapigana nao akiwa pamoja na malaika zake" (12:7). Huko mbinguni, Shetani aliwaunganisha malaika wote walioanguka kwa kuwadanganya ili wa inuke kwa ku mpinga Mungu kwa sababu alitaka kuchukua nguvu mamlaka yote ya Mungu na kuchuka kiti cha enzi.

Lakini shetani alipoteza vita hivyo vya kwanza, na Mungu akamtupa nje yeye pamoja na malaika wote waliompinga kutoka mbinguni. Shetani alikuwa amewadanganya wale malaika na wakati Mungu aliumba watu, aliamua kuwadanganya pia.

Uasi wa Shetani haukumushangaza Mungu. Hata kabla ya msingi wa ulimwengu, Mungu alipanga mpango wa vita vya kuishinda Ibilisi. Bwana aliumba mwanadamu kwa sanamu yake na akamruhusu awe na hiari ya uhuru - kisha akamtuma Mwanawe, Yesu, kuwakomboa watu wote!

Yesu anangojea uvumilivu wa mavuno ya mwisho ili aingizwe ndani, lakini mpaka kuja kwa Bwana, ndio tutaweza kuishi maisha ya ushindi: "Sisi ni zaidi ya washindi kupitia Yeye ambaye aliyetupenda" (Warumi 8:37).