"WALIMULILIA SAANA BWANA"
Biblia inaahidi kwamba inawezekana kuelewa upendo wa Bwana. Je, ni ufunguo gani? Mfalme Daudi akasema, "Aliye na hekima ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za Bwana" (Zaburi 107:43).
Daudi alipata ufunuo wa kushangaza kwa neema ya Mungu, na moyo wa kusamehe. Na aligundua tu kwa kuangalia rekodi ya Mungu ya zamani ya kushughulika na watoto wake wapendwa. Daudi anaripoti kwa hii njia:
"Waliona njaa, waliona na kiu, nafusi yao ilikua ikizimia ndani yao, wakamlilia Bwana katika dhiki zao, akawaponya nashida zao, akawaongoza kawa njia ya kunyoka…na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, na maajabu yake kwa wanadamu!" (Zaburi 107:5-8).
Wakati wana wa Israeli walipotea mbali na Bwana, wakawa na njaa, wakaona kiu na kupotea kwa sababu ya dhambi. Lakini basi wakaliliia Bwana, na nini kilichotokea? "Maana hushibisha nafsi yenye shauku, na nafsi yenye njaa huijaza mema" (107:9).
Hata hivyo waliasi na kurudi nyuma, wakianguka chini kabisa. Tena tunasoma: "Wakamlilia Bwana katika dhiki zao ... hulituma neno lake, huwaponya" (107:19-20).
Hatimaye, watu wa Mungu walikuja tena na uwezo wao wa mwisho wa kufikili. Dhoruba ilio haribu na nafsi zao ziliyayushwa na shida: "Kisha wanamlilia Bwana katika taabu yao, na anawaondoa katika taabu zao, huwafungua dhoruba, na mawimbi yake bado" (107:28-29).
Daudi alijibu kwa ufunuo huu, "Angalia jinsi moyo wa Mungu unavyogeuka kwa urahisi.Hakika, kwa haraka anaitikia kilio cha watoto wake ... Hakuna huruma kwa huruma zake."
Mpendwa, huhitaji kuendelea na uchungu na hatia. Badala yake, nenda kwa Bwana, kilio na kumkiri kwake. Yeye ni Baba mwenye huruma ambaye huguswa na kila kilio chako.