WATUMISHI WALIOGUSWA NA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Danieli akashuhudia, "Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu" (Danieli 10:10). Neno la "kuguswa" hapa linamaanisha kushikilia kwa ukali. Danieli alikuwa akisema, "Mungu alipoweka mkono wake juu yangu, inaniweka juu ya uso wangu; kugusa kwake kunanijaza kwa haraka kumtafuta kwa kila kitu kilicho ndani yangu."

Watumishi walioguswa na Mungu wana uhusiano wa karibu na Bwana. Wanapokea mafunuo kutoka mbinguni na kufurahia kutembea na Kristo ambayo wengine wachache hufanya. Wakati wowote Mungu akigusa maisha ya mtu, mara nyingi huyu huanguka kwa magoti na huwa mtu wa sala, anayemtafuta Bwana. Mara nyingi nimejiuliza kwa nini Mungu huwagusa watu fulani tu kwa mbio hii. Kwa nini watumishi wengine wanakuwa watafutaji wake wenye njaa, wakati watu wengine waaminifu wanakwenda kinyume ya njia zao?

Danieli, mtumishi aliyejitoa, aliguswa na Mungu kwa njia isiyo ya kawaida. Kulikuwa na watu wengi wema, waabudu wanaomtumikia Bwana katika siku ya Danieli. Hawa ni pamoja na Shadraki, Meshaki na Abednego na makumi ya maelfu ya Waisraeli wengine ambao waliendeleza imani yao wakati wa utumwa huko Babiloni.

Kwa hiyo, kwa nini Mungu aliweka mkono wake juu ya Danieli na kumgusa kama alivyofanya? Kwa nini mtu huyu alikuwa na uwezo wa kuona na kusikia vitu mtu mwingine hangeliweza kusikia? "Nami, Danieli, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja name hawakuyaona maono haya" (Danieli 10:7). Maono Danieli alioyaona alikuwa Yesu mwenyewe, wazi kwa wazi. Kwa kweli, ilikuwa ni maono sawa nay ale yaliyopewa Yohana kwenye kisiwa cha Patmos (angalia Ufunuo 1:13-15).

Bwana alijifunulia Danieli kwa njia aliyofanya kwa sababu kijana huyu alikuwa amevumilia na shauku ya kujua moyo wa Mungu. Pia, Mungu aliamua wakati uliokuja kutoa ujumbe kwa ubinadamu uliopotea na alihitaji sauti ya kuzungumza ujumbe wake.

Leo, Bwana anatafuta wale ambao walio na hamu kubwa ya kumjua na wataomboleza juu ya hali ya maadili katika jamii yetu - wakati pia wana shauku yakutazama kuja kwa Kristo.