WITO WA KUWEKA MIOYO YETU JUU YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Yeremia nabii alikuwa mtu ambaye aliweka moyo wake kwa kumtafuta Bwana, na Neno la Mungu lilimjia. Mara kwa mara tunasoma kuhusu nabii, "Neno la Bwana lilimjia Yeremia."

Wachapishaji wengi wanamwita Yeremia ni nabii mwenye kilio, na hiyo ilikuwa kweli kwa yeye. Lakini pia alituletea injili yenye furaha zaidi, yenye sifa kubwa katika Agano Jipya. Baada ya yote, alitabiri utukufu wa Agano Jipya: "Nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuaacha, ili niwatendee mema" (Yeremia 32:40). "Nami nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono, na watu wangu watashiba kwa wema wangu, asema Bwana" (31:14).

Sasa, hiyo ni habari njema! Agano Jipya ni kamili yenye kujaa huruma, neema, furaha, amani na wema. Lakini, historia ya kila maneno ya Yeremia hapa inajumuisha kuvunjika kwa kina.

Yeremia aliandika, "Oh nafsi yangu, oh nafsi yangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamanza; kwa sababu umesikia, ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta mshindo wa vita" (4:19).

Yeremia alikuwa akilia na machozi matakatifu ambayo hayakuwa yake mwenyewe. Hakika, nabii kweli alimsikia Mungu akisema juu ya moyo wake mwenyewe uliovunjika. Kwanza, Bwana alimwambia Yeremia kwamba angeenda kutuma hukumu juu ya Israeli. Kisha akamwambia yule nabii, "Kwa milima nitalia na kulalamika, na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo" (9:10). Neno la Kigiriki la "maombolezo" hapa linamaanisha kulia. Mungu mwenyewe alikuwa akilia juu ya hukumu iliyowajia watu wake.

Bwana anashiriki nasi mawazo yake kabisana fikira zake. Tunaishi katika nyakati za maisha na kifo, sasa na ninawahimiza kuweka moyo wako kumtafuta Mungu kwa bidii na uamuzi. Kisha nendea Neno lake pamoja na upendo unaoongezeka na hamu. Atukuwa mwaminifu kwa Neno lake na atawaongoza katika yote ambayo anataka kukufunulia.