YESU HAWEZI KUSHINDWA KAMWE

Gary Wilkerson

"Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja name popote nilipo, wapate kuona utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu" (Yohana 17:24, msisitizo wangu). Yesu aliwaombea wanafunzi wake - na hilo linajumuisha sisi. Alimwomba Baba ili tuweze kuona utukufu wake, inamaanisha kwamba tunamjua.

Kwa nyakati fulani katika Agano la Kale, Yesu alijifunua kwa mufano wa mwanadamu au wa malaika, kwa matokeo mbali mbali. Kwa mfano, kiuno cha Yakobo kilivunjika wakati alijaribu kupigana na Bwana. Na Musa alipomwambia Mungu, "Nakusihi unionyeshe utukufu wako" (Kutoka 33:18), Bwana akamwambia, "Lazima Mimi nifunike uso wako na kukuficha nyuma ya mwamba, na kisha unaweza kuona tu baada ya kufuata uwepo wangu." Kwa maneno mengine, alipaswa kulinda Musa kutoka kwa ufunuo kamili wa yeye mwenyewe.

Katika Agano Jipya, mtume Yohana aliposikia sauti ya Bwana na kupokea Ufunuo akiwa kwenye kisiwa cha Patmos, akaanguka juu ya uso wake. Jibu la kawaida la wanaume na wanawake walipomwona Yesu ilikuwa ni kuungama na kushangaa. Nashangaa nini kingetokea ikiwa tungemwona akiwa katika uzuri wake wote na utukufu kama Mose au Yohana walivyomuona.

Ukweli ni kwamba, Yesu ni mzuri sana zaidi kuliko matumizi yetu kwa kawaida ya neno linalotumiwa kwa maelezo. Tunaona kwamba mtu ni anapendana au ni mzuri, lakini Yesu ni zaidi mbali ya hayo. Yeye ni mutukufu, wa ajabu, tofauti, wa kipekee, maalum. Yeye pia ni mwepesi, mwenye fadhili, mwenye thamani, mwenye utukufu. Yeye ni wa ajabu, mwenye nguvu, mwenye nguvu, mwenye uwezo, mwenye busara, bora kuzidi watu wote. Na yeye hashindwi kamwe!

Hata katika hali yake ya kibinadamu, Yesu aliendelea kuwa huru, mmoja na Mungu (angalia Wakolosai 2:10). Fikiria baadhi ya sifa zake nzuri: kamili ya haki (Yohana 8:16); Mwenye haki kabisa (Yohana 8:46). Na yeye ni upendo (Yohana 13:34) - upendo ambao hauwezi kutambulika.

Sisi hatufai kabisa upendo huu, lakini huu ndiyo uzuri wa Mwokozi wetu wa kushangaza, asiyeweza kulinganishwa. Mpe sifa sasa kwa dhabihu yake isiyoweza kusemekana na zawadi ya wokovu.