YESU TAYARI ANATAWALA KAMA MFALME!

David Wilkerson (1931-2011)

Nebukadneza akaweka sanamu ya ngo’ombe ya dhahabu huko Babiloni na akaomba iabudiwe. Kila afisa, kila kiongozi na kila raia katika mikoa mia moja ya Babiloni walipaswa kuanguka chini mbele ya mungu huu au kukabiliana na kifo – kwa kuchomwa hai ndani ya tanuru. Hata hivyo, Wayahudi watatu waaminifu katika ufalme walikataa kuinama, na mfalme akawa na hasira na akawatupa kwenye tanuru la moto. Lakini Bwana akashuka na kuwakomboa watumishi wake, na mfalme akasema, "Na ahidimiwe Mungu wa Shadraki, Meshaki, na Abednego, aliyemtuma malaika wake na kuwaokoa watumishi wake waliomtumainia, waliolikaidi neno la mfalmee, na kutoa miili yao, ili wasimtumikie mungu mwingine wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe!" (Danieli 3:28).

Uislam ni dini ambayo inatishia ulimwengu wote kwa kutaka watu wafanye ibada ya mungu wawo, Allah. Ni aina ya Babiloni, pamoja na mashirika ya kigaidi wanadai, "Inamia Allah au kama hafanyi hivy, sisi tutalipua ndege yako, tutalipua miji yenu, treni, mabasi na njiya za kupitia chini ya ardhi. Tutawafanya mateka, tutawatesa na kuwakata vichwa. Allah atatawala ulimwengu na Uislam utatawala."

Kuna ghadhabu na asila inayoongeze katika mioyo ya watu waovu dhidi ya jina la Yesu. Tunajua kwamba jina la Yesu daima limechukiwa na watu waovu, lakini sasa chuki imegeuka kuwa hasira kutoka kwa ma pepo. Kwa kweli, jina lake polepole na kwa kiasi kikubwa kufutwa kutoka kwa jamii, na kwa mamlaka ya kisheria katika mataifa duniani kote.

Kuna ghadhabu ya Shetani inayoongezeka dhidi ya kila mfuasi wa Kristo. Ikiwa unakaribia karibu na Bwana, basi unakabiliwa na ghadhabu kamili ya shetani mwenye hasira. Hata hivyo, silaha yetu kuu kwa kutia chini ngome za Shetani, ni Neno la Mwenyezi Mungu. Hatufadhaike juu ya vita ambavyo Shetani inaonekana kuwa ameshinda. Vita tumwo ndani ni vya milele na milango ya Jahannamu hayatashinda kanisa la Kristo. Baba yetu ametangaza: Yesu tayari anatawala kama Mfalme!