YEYE ANATUOMBA KUFUATA TU
Hakuna kitu kinachosisimua kama kutembea kila siku na Roho Mtakatifu. Kuhamia na kupumua nguvu za Mungu. Kusikiliza kwa sauti inayokuja kwenye akili yako, kisha kuitii chochote angependa. Kwenda popote atakapokuambia kwenda. Na kusema kile anachokuambia kusema. Kumtumikia mahari popote anapokuweka katika njia yako. Kunywa kutoka kisima cha ujuzi wake kwa kuchangia hilo ndani ya moyo wako na mawazo yako.
"Roho hutoa uzima; mwili haufai kitu. Maneno niliyowaambia – ni roho na uzima" (Yohana 6:63).
Ninajaribu kamwe kutouliza njia za Roho Mtakatifu, kutokuwa kamwe na shaka kuhusu ndani ya muonekano wake, kamwe usisite akuache kukuongoza. Watu wengi wanajaribu kuelimisha Roho Mtakatifu juu ya kile anapaswa kufanya, lakini Roho wa Mungu hatowe jibu kwako na mimi au kutuuliza chenye tunafikiri kuhusu njia zake. Yeye anatuomba tu kufuata.
Sala yenye nguvu zaidi na yenye ufanisi inaweza kusema, "Yesu, ninaachilia maisha yangu kwa kazi ya Roho Mtakatifu wako. Sina mipango yangu mwenyewe, hakuna ajenda, hakuna malengo ya uchaguzi wangu mwenyewe, hakuna tamaa imewekwa ndani yangu kuhusu mambo yako. Ninakataa Shetani kushikilia maisha yangu na dhambi ambazo zinanifanya kuwa mtumwa. Nionyeshe mahari unataka niende, kitu unachotaka mimi nifanye, mwenye unataka nione, na chenye unataka mimi niseme. Hivi sasa sitaongeza tena kuweka mpaka katika kazi yako ndani ya maisha yangu. Nishike! Nitie changamoto! Nitumie! Niongoze! Nifanye chombo cha Roho wako!"
Badala ya kutumia maisha yako kuomba kwa ajili ya baraka, omba Mungu akutumie wewe kubariki wengine. Badala ya kujitahidi kuwa na maisha mazuri na utajiri na kula vizuri. Badala ya kutafuta miujiza, basi acha Mungu ageuze maisha yako kuwa uzima wa kuonekana, upumuwe miugiza ya mapenzi yake.
Hiyo ndiyo njia ya kweli yakufanya kitu kinachoonekana duniani kwa ajili ya Kristo na kuacha urithi wa kudumu.
Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka ( Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).