UPENDO WA BWANA WA KUADIBU
Kwa sababu Mungu anakupenda, atafanya kazi ya kukusafisha. Unaweza kuhisi mishale ya Mungu katika nafsi yako kwa sababu ya dhambi zako, lakini unaweza kuita upendo wake wa kuadibu. Hutasikia hasira yake kama watu wa mataifa. Fimbo ya Bwana itatumika kwa mkono wa upendo.