KUFUATA HEKIMA YA MUNGU
“Malkia wa Kusini atasimama katika hukumu pamoja na kizazi hiki na kukilaani; kwa maana alikuja kutoka miisho ya dunia kusikia hekima ya Sulemani; na kwa kweli aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa” (Mathayo 12:42).
Malkia wa Sheba alisumbuka sana katika nafsi yake na maswali yote makubwa ya maisha - juu ya Mungu, siku zijazo, kifo - na alitamani majibu. Hata hivyo hakuna utajiri, umaarufu au ushauri unaweza kujibu kilio cha roho yake. Kisha akasikia juu ya Mfalme Sulemani, mtu mwenye hekima zaidi aliyewahi kuishi.