AHADI BORA ZAIDI, NA KUISHI KWA MATUMAINI

David Wilkerson (1931-2011)

Chini ya Agano la Kale, ahadi kwa Waisraeli kwamba Mungu atawabariki ikiwa wanaheshimu ilikuwa ni yote waliokuwa nao. Lakini leo, chini ya Agano Jipya, tuna "ahadi bora zaidi." "[Kristo] kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lilioamriwa juu ya ahadi zilizo bora" (Waebrania 8:6).

Hii "ahadi bora" inamaanisha sisi wote tutamjua. Hatuna tena kuhani mkuu ambaye huenda mbele ya Mungu. Hapana - pazia ilichaniwa mala mbili ili tuweze wote kuja mbele ya Mungu!

Zingatia yale yote Bwana ametuahidi sisi:

KUCHAGULIWA KWA AJILI YA MUNGU

Gary Wilkerson

Katika usiku uliotangulia kabla ya kusulubiwa kwake, katika jioni ya mwisho, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena, bali ninyi mnaniona" (Yohana 14:19). Tamko gani la kuvutia amabalo Yesu anafanya. Mmoja wao aliuliza, "Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?" (14:22).

KUINUKA KATIKA UMOJA

Nicky Cruz

Nini ikiwa Mwili wa Kristo kwa ujumla unaweza kuja pamoja kwa umoja, kuacha tofauti zetu za maoni na migogoro yetu ya kijamii na mafundisho, na kutazama lengo moja tu – la kufikia waliopotea? Nini kama tuliomba Roho Mtakatifu kuponya majeraha na kuleta msamaha kwa mioyo na roho zetu, kusahau ya zamani na kuzingatia ya baadaye? Ni ufufuo gani wa kiroho ambao ulimwengu unaona wakati wanatuwona sisi, tukisimama pamoja mbele yao tukiwa na umoja?

KUPENDWA KWA KIMAAJABU NA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Baada ya miaka ya huduma unaweza kujipata bado unafundishwa na Bwana. Hatuachi kamwe kujifunza kuhusu kufuata mwelekeo wake wazi, hasa wakati anatuongoza kwenye maeneo magumu. Mimi bado ninajifunza kutosema, "Hiyo ndivyo ilvyo, Mungu. Nimetosheka. "Badala yake, ninajifundisha mwenyewe kusema," Bwana, sioni njia ya mbele; Sijui ambapo nitapata neema ya kupitia hii. Lakini uliahidi kuwa nguvu zangu."

BWANA "ANAJUA HARI YAKO"

David Wilkerson (1931-2011)

Je! Umewahi kuwa na shida ya kumtii Mungu kwa sababu unataka kweli kuendelea na kufanya kitu peke yako? Ikiwa ndivyo, ninaweza kukuhimiza tu kuchunguza wito wako. Fanya kile ambacho Mungu anakuambia kufanya na kwenda hasa ambapo anaongoza. Ikiwa uko hapo sasa, wewe ni amani. Lakini ikiwa huna amani, huenda ikawa kwa sababu hutumii Bwana kwa namna unapaswa kuwa.

MAOMBI ANAOJIBU ZAIDI

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati mwingine Mfalme Daudi alimwomba Mungu amokoe kutoka kufa, na Mungu akajibu sala yake: "Alikuomba uhai, ukampa - mda mrefu wa siku nyingi" (Zaburi 21:4). Lakini Mungu aliendelea zaidi katika kujibu sala ya Daudi. Sio tu alimpa uzima, naye pia akaweka taji juu ya kichwa chake na kumfanya awe mfalme wa Israeli.

Baada ya Mungu kumfanya Daudi mfalme, akamumwangia heshima na utukufu juu yake. "Umemvika taji ya dhahabu safi kichwa chake. . . Heshima na adhama waweka juu yake" (2:3 na 5). Na juu yake, Mungu aliongeza furaha kubwa: "Wamufurahisha kwa furaha ya uso wako" (21:6).

BILA MTU WA KATIKATI

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo wengi wanataka kusikia na kujua sauti ya Mungu na kwa hakika Mungu anataka kuzungumza na watu wake. Lakini waumini wengi waligeuza kuwa sanamu – wa tumishi wanaoeshimika, mwalimu au minjilisti - ambaye anaongea mambo mema tu kwao. Ili kujua sauti ya Baba, mtu lazima aende moja kwa moja kwake bila mtu wa kati.

YESU ALISHIKIRIA LENGO LAKE

Gary Wilkerson

Kama wafuasi wa Kristo, tunapaswa kuwa makini kuanguka katika mtego unaopendwa na Shetani: kuingizwa katika hali mbaya ya utamaduni na ya kisiasa ambayo imezagaa katika dunia yetu. Kwa kuwa Shetani hufanya dunia kuwa hasira zaidi kwa Wakristo, yeye anajaribu kutufanya tukasirike na kulipiza kisasi. Kwa maneno mengine, anataka kuchukua nafasi ya amani yetu ndani ya Yesu kwa ugomvi, na kutufanya sisi kupinga mashambulizi ya mateso badala ya kuvumilia kwa ajili ya injili.

NINI KINGINE ISIPOKUWA UPENDO

Jim Cymbala

Maisha ya upendo ndiyo njia pekee ya "kumpendeza Mungu kila njia" (Wakolosai 1:10). Kwa kuwa Mungu ana roho ya kiutu ya kuhisia, hupata furaha na huzuni kama sisi. Maneno na vitendo vyetu vya kila siku vinaweza kumfanya hasira au kumfanya afurahi juu yetu na kuimba. Nini mawazo ya kushangaza! Leo wewe na mimi tunaweza kumpendeza Mungu wa ulimwengu. Kwahiyo yeye anaelewa Zaidi na zaidi, mwenye nguvu, yeyote, na kila mtu, moyo wake unaweza kuguswa na matendo yetu ya upendo, hata katika shughuli za kawaida. Nini kingine, ila upendo unaweza kumpendeza Mungu wa upendo?

PENDA MUNGU, PENDA WATU

David Wilkerson (1931-2011)

Kutoka mwanzo wa misingi ya dunia, Mungu alitabiri mwili wa waumini waliounganishwa na Mwanaye. Yesu anashuhudia, "Nilikuwa furaha ya kila siku ya Baba yangu, furaha ya kuwa kwake. Na sasa wote wanaogeuka kwangu kwa imani ni furaha yake pia" (angalia maneno haya ya kinabii ya Kristo katika Mithali 8:30-31).

Tunaonyeshaje upendo wetu kwa Yesu? Yohana anajibu: "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito"(1 Yohana 5:3).