MATUNDA YA UPENDO WA BABA
Upendo wa Mungu ulitolewa kwetu kupitia Yesu Kristo. Kwa mujibu wa Yohana, upendo wote wa Mungu unakaa ndani ya Yesu: "Kwakua katika utimilifu wake sisi sote tulipokea” (Yohana 1:16). Unaweza kuuliza, "Ni jambo gani muhimu kwa kujua kwamba upendo wa Mungu ulitolewa kwetu kupitia Kristo? Hii inathirije maisha yetu ya kila siku?"