MAANA YA UPENDO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati mume (au mwanamke) wa Mungu akiwa kwenye matengenezo, majeshi ya adui atakuja kwake kwa ghadhabu kubwa.

Je, unahonja kikombe kichungu cha maumivu, kudumu saa ya kutisha ya kutengwa na ya kuchanganyikiwa? Ikiwa ndio, nawahimiza kusimama kwa imani: "Kwamaana namujua yeye niliye mwamini, nakusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile" (2 Timotheo 1:12).

SEHEMU NGUMU ZAIDI ZA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alisema huko Gethsemane, "Roho yangu ina huzuni nyi kiasi cha kufa" (Mathayo 26:38). Je, unaweza kufikiria Mwana wa Mungu akivumilia usiku wa kuchanganikiwa? Je, hakujua kwamba alikuwa karibu kudai ushindi wote juu ya kuzimu na kifo? Je, hakuwa na hisia ya ukoo ya muongozo na hatimaye, akijua kama Baba alikuwa pamoja naye?

Imesemwa na vizazi vya Wakristo kwamba sehemu ngumu zaidi ya imani ni nusu saa ya mwisho. Ninataka kuongeza neno hapa kwamba usiku mubaya wa kuchanganikiwa mara nyingi huja kabla ya ushindi, haki kabla ya giza kuvunja na mwanga hutokezea alfajili.

UKWELI, WA MAISHA MENGI

Gary Wilkerson

Wakati Roho inatufanya tuongeye kwa upendo, tunapaswa kufanya hivyo. Hivi karibuni wakati tulikua tunakula chakula cha mchana na mke wangu, nilihisi nia ya kumwambia mmoja wa watumishi wa mugahawa katika eneo letu kwamba Yesu alimpenda. Hakuwa na jibu lakini baadaye nikamwona akiwaambia wafanyakazi wengine kile nilichosema, ambacho hatukutalajia kukiona. Kisha jambo la kushangaza lilifanyika. Tulipokuwa tukiondoka, mhudumu tofauti alinisimamisha na kuwuliza kama ningependa kuomba pamoja naye!

RATIBA YA MUNGU

Carter Conlon

Wakati Mungu anasema, "Nitatumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wangu," mara nyingi tunasahaulika kwamba upanga hautengenezewe kutoka kwenye mti, bali hutengenezwa kuta kwenye kiyayusho. Kutakuwa na joto, kunyoosha, kukunja, na kunoa tena kutazama tena. Yote ni muhimu, na itachukua muda. Hata hivyo katika mchakato huo, tunasema, "Bwana, nilifikiri kama unasema unaenda kutumia maisha yangu, lakini yote ninayofanya nimejikuta nikipitia kwenye moto. O, Yesu, nisaidie!”

NDANI YA MACHO YA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Ninaposema imani kamili katika Kristo, simanishi tu katika nguvu zake za kuokoa lakini pia katika uwezo wake wa kuweka. Tunatakiwa kuamini Roho wake ili atuhifadhi na kutufananisha na mfano wa Kristo.

Wakati mmoja ulikuwa mbali, ukatwa na Mungu kwa kazi mbaya. Ulifanya kazi gani nzuri ya kufanya mambo sawa na yeye? Hakuna! Hakuna aliyewahi kufanya au kujitunza mwenyewe. Tunaletwa katika utakatifu wa Kristo kwa imani peke yake, kama tunavyoamini katika kile ambacho Neno la Mungu linasema: "Ikiwa mmekuwa ndani ya Kristo, nanyinyi ni watakatifu kama yeye yu mtakatifu."

UTEGEMEZI KAMILI JUU YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Tunajua kwamba Mungu aliwaokoa Israeli kabisa. Katika kijiti cha moto, Musa alikuwa akiandaliwa kumwamini Mungu kuleta kazi hiyo ya utukufu. Angejifunza kitu kuhusu asili ya Mungu ambayo baadaye itamsaidia kumtegemea Bwana kuifanya yote. Nini kipengele hicho cha asili ya Mungu? Utakatifu wake!

KIJITI KINACHOWAKA

David Wilkerson (1931-2011)

Musa alikuwa peke yake juu ya Mlima Horebu akichunga kondoo za baba mkwe wake wakati alipoona mbele yake kitu cha ajabu kilicho ingiya ndani ya mawazo yake - kijiti kilikuwa cha moto. Alipokuwa akisonga mbele ili atazame kwa kusogelea, Mungu alimwita nje ya kichaka.

NJIA YA KUELEKEA UTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu Kristo, Mwokozi wetu, anasimama peke yake katika utakatifu kamili. Kwa sababu Yesu peke yake ni mtakatifu na mkamilifu, Mungu hamtambui mtu mwingine yeyote. Kwa hiyo, ikiwa tutapokewa daima na Baba wa mbinguni, lazima tuwe ndani ya Kristo, kwa neema tu ya Kristo na kwa kupitia sifa isiyofaa kwetu wenyewe.

MBALI NA UPENDO WA YESU

Gary Wilkerson

Waanadini wana tabia ya kuzingatia giza badala ya nuru. Nasikia Wakristo wengi wanaachilia maneno maumivu: "Utamaduni ni wa kulaumiwa," au "Serikali ni yakutenda kosa," au "Kundi hilo lina ushawishi mbaya kwa maslahi yawo maalum," Ikiwa unatembea kama Yesu alivyofanya, hutaweza kulaani giza kwa sababu wewe unaangazia nuru yenye unaleta. Hebu aca nionyeshe.

SABABU YA MUNGU KUONYESHA NGUVU ZAKE

Nicky Cruz

Katika sura ya tatu ya Matendo, baada ya Petro na Yohana kumponya mwombaji kiwete kwenye lango lakuingia ndani ya hekalu, wachache waliokuwa wakiangalia walisimama mbele. Walikuwa wamemjua mtu miaka mingi, na uponyaji haukuweza kuepukika. Watu waliwauliza wanafunzi kuhusu hilo, Petro akawaambia, "Enyi waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi? Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu” (3:12-13).