DHAMBI YA KUTOAMINI

David Wilkerson (1931-2011)

Kutoamini kunahuzunisha moyo wa Mungu kuliko dhambi nyingine yoyote. Sisi Wakristo tunalia dhidi ya dhambi za mwili, lakini Mungu anahusika na dhambi za moyo - kuwa na mashaka juu ya Neno lake au kuwa na maswali juu ya uaminifu wake. Masuala halisi ya maisha na kifo ni mengi zaidi na jinsi mtu anavyofikiri kuliko kile anachofanya.

USALAMA KATIKA KILA HALI

David Wilkerson (1931-2011)

"Usiogope hofu ya ghafula, wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, naye atakulinda mguu wako usinaswe" (Mithali 3:25-26).

Watu wengi leo wanauliza maswali ambayo hawana jibu la uhakika. Je, kutakuwa na wasiwasi hivi karibuni? Je, tunakabiliwa na dhoruba kubwa ya kiuchumi ambayo mawaziri wengi na watalamu wa uchumi wameonya?

ILI NIWEZE KUJUA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu alimpa Musa maagizo ya kutisha: "Haya, ondokeni, katokeni hapo wewe na hao watu uliowaleta wakwee  kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, niliposema, 'Nitakipa kizazi chako nchi hii.' Nami nitamtuma Malaika wangu aende mbele yako . . . kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwasababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia" (Kutoka 33:1-3).

KRISTO ANAKUJA!

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Danieli alitabiri kampuni ya watu wa siku za mwisho iliyo na hekima na ufahamu katika mambo ya Mungu - waliosalia waliojitakasa, waliopimwa ambao wataelewa Neno lake. "Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa" (Danieli 12:10).

HII NI NIZAWADI YA AJABU KUTOKA KWA NEEMA

Gary Wilkerson

"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu" (Waefeso 2:8-9, ESV).

Maisha yetu katika Kristo huanza kwa neema, inaendelea kwa neema, na itaisha kwa neema. Mara tunapofahamu jambo hili, maisha yetu yatakuwa na uhuru badala ya utumwa; kwa furaha badala ya uchovu; kwa furaha badala ya hofu. Kutumia muda mbele ya Mungu kutaonekana kama zawadi ya furaha kwa sababu tutakuja kuelewa kwamba sisi si watumishi tena lakini marafiki wa Yesu.

WAKATI MUNGU ANAKUWA KIMYA

Carter Conlon

Tunapoangalia safari yake, tunaona bilashaka Mfalme Daudi alianza kwa nguvu. Roho Mtakatifu alikuja juu yake, akimfanya kushinda simba na dubu, na hatimaye jitu Mfilisti. Ilionekana kama siyo mwisho wa kile ambacho Mungu angeenda kufanya kupitia maisha yake, mpaka wakati wa utulivu ulikuja. Ghafla Mungu hakuwa akizungumza jiya aliyotumia, na Daudi akaanza kupoteza imani. Alipoteza imani katika maneno ya zamani ya Mungu juu yake, ambayo ilimfanya ajaribu kuongoza maisha yake kwa hekima yake mwenyewe na kutatua matatizo yake kwa nguvu zake mwenyewe (angalia 1 Samweli 27:1-3).

SALA ZA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Sala ni siri ya ukuaji wa kiroho, lakini ikiwa tunakwenda kwa kiti cha enzi tu kwa ajili ya kuimarisha na mahitaji yetu binafsi, tunakuwa na ubinafsi. Biblia inatuonyesha kwamba hatuwezi kuacha kuomba sana kwa mahitaji ya wale walio karibu nasi na kutupa mifano ya "sala zenye manufaa" (angalia 2 Wakorintho 1:11).

SALA LA USAIDIZI

David Wilkerson (1931-2011)

Kila mchungaji, mhubiri na muinjilisti anahitaji wasaidizi katika sala lenye kuendelea ili awaombee. Ninawahakikishia kwamba kwa miaka mingi nimekuwa nikibebwa kwa kuombewa na watumishi waaminifu.

Maandiko yanasema kwamba Petro alipokuwa amefungwa gerezani, "Kanisa liliomba Mungu mara kwa mara kwa ajili yake" (Matendo 12:5). Mungu alimuokowa Petro kwa muujiza kupitia sala ya usaidizi.

UZURI WA KUSIFIWA

David Wilkerson (1931-2011)

Katika Zaburi, Daudi anapanua uzuri wa Mungu katika kuwabariki wale wanaomwamini.

"Jinsi zilivyo nyingi fadhili zako ulizowawekea wakuchao; ulizowatendea wakukimbiliao mbele ya wanadamu! Utawasitiri na fitina za watu katika sitara ya kuwapo kwako; utawaficha katika hema na mashindano ya ndimi." (Zaburi 31:19-20).