WATIMOTHEO WAKO WAPI?
Ilikuwa kwa Wakristo wa Filipi kwamba Paulo alianzisha ukweli huu kwanza, "Iweni na nia hii ndani yenu ambayo pia ilikuwa ndani ya Kristo Yesu" (Wafilipi 2:5).
Paulo aliwaandikia ujumbe huu wakati alikuwa gerezani huko Roma, akitangaza kwamba alikuwa na akili ya Kristo na akiachilia mbali sifa yake ya kuwa mtumishi wa Yesu na kanisa lake. Kisha akaandika, "Natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili mimi pia nifarijiwe ninapojua hali yenu" (Wafilipi 2:19).