MUNGU ANAPORUHUSU UPINZANI
Katika siku ambazo Wafilisti walikusanyika kupigana na Israeli na magari 30,000, wapanda farasi 6,000 na watu wengi kama mchanga wa pwani, Mfalme Sauli na wanaume wa Israeli waligundua kuwa walikuwa hatarini na wakaanza kujificha katika mapango na mashimo. Maandiko yanasema kwamba wengine walimfuata Sauli huko Gilgali, wakitetemeka. Walakini kulikuwa na mmoja ambaye hakupatikana kati ya waoga. Yonathani, mwana wa Sauli, akamgeukia yule mchukua silaha zake na kusema, "Njoo, tuvuke hadi kwenye kambi ya hawa watu wasiotahiriwa; yawezekana Bwana atatufanyia kazi.