JAMBO SAHIHI KWA WAKATI UNAOFAA
Musa alikutana na Mungu, mara nyingi kwa mtindo wa kushangaza; Neno linatuambia kuwa "Malaika wa Bwana akamtokea katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti" (Kutoka 3:2). Wakati huo Mungu alimwita Musa aongoze wana wa Israeli kutoka utumwani wa Misiri na ilimbidi atoe maisha yake ili kufuata mwongozo wa Bwana. "Basi Musa akaenda, akamrudia Yethro baba mkwe, akamwambia, Tafadhali naomba niende nikarudi kwa ndugu zangu walioko Misri"… Ndipo Yetro akamwambia Musa, Nenda kwa amani” (Kutoka. 4:18-19).