BWANA, KWA NINI?

David Wilkerson (1931-2011)

Sio dhambi kwa muumini kuuliza kwa nini; hata Bwana wetu aliuliza swali hili alipokuwa akipigwa na maumivu msalabani (angalia Mathayo 27:46). Wakati mwingine tunaweza kulia, "Bwana, kwa nini unanipisha kwa njia hii? Najua haitoki kwa mkono wako, lakini bado unaruhusu shetani aendeleye kunisumbua. Je, ni lini hayo ataisha?"

"TUTAFANYA HILO KWA NIYABA YETU"

David Wilkerson (1931-2011)

Mtume Isaya alisema juu ya Israeli: "Ole wao watoto waasi; asema Bwana, watakao mashauri lakini hawataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha Roho yangu; wapate kuongezeka dhambi juu ya dhambi " ( Isaya 30:1). Neno la Kiebrania, ole hapa linamaanisha huzuni na maumivu juu ya kile ambacho Mungu anaelezea kama uasi, maana ya kurudi nyuma, ukaidi, kugeuka.

KUSONGA MBERE KARIBU NA YESU

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana anajitayarisha kumwaga Roho wake juu ya watu wake katika siku hizi za mwisho na najua unataka kuwa na sehemu ndani yake. Ili jambo hili lifanyike, lazima tuwe karibu na yeye - katika ibada yetu, utii na bidii. "Mkaribie Mungu naye atawakaribia ninyi" (Yakobo 4:8).

RUDIA NA UTAFUTE USO WAKE

Gary Wilkerson

Waumini wengine huomba tu wakati wanapoadhibiwa na Mungu. Wao wakishawishiwa na hujisikia vibaya na ndio wanaanza kuanza kuomba, na kisha hatua kwa hatua kusahau kuomba tena. Biblia inasema, "Lakini watu wangu waminisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu" (Yeremia 2:32).

SI KITU CHA BULE KUTOKA KWA ONYO

Carter Conlon

Mtume Petro alitoa neno la onyo kwa watu wa Mungu: "Wapendwa, musione kuwa nia ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba nikitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe" (1 Petro 4:12-13).

Aina hii ya ujumbe inaweza kuwa ngumu sana kukumbatia wakati wa amani. Watu wa Mungu wanaweza kukua kwa urahisi na kuwasahau kuwa wanaishi katikati ya jamii ambayo inaweza ghafla, hata kwa ukali, inapingana na Kristo na wafuasi wake.

UTUKUFU WAMILELE UNAOONGEZEKA

David Wilkerson (1931-2011)

Akawaambia, "Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimwa, na tena mtazidishiwa" (Marko 4:24).

Yesu alijua maneno haya kuwa anaweza kusikiwa kama ya ajabu kwa masikio ya kiroho, kwa hiyo alianza ujumbe wake kwa kusema, "Mtu akiwa na masikio ya kusikia, asikie" (4:23). Alikuwa akituambia, kwa kweli, "Ikiwa moyo wako ni wazi kwa Roho wa Mungu, utaelewa kile nitakachokuambia."

ISIWE MUJINGA, YESU ANATAWALA

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu anawalazimisha mataifa ya ulimwengu. Biblia inatuambia, "Atawala kwa uwezo wake milele; macho yake yanaangalia mataifa; waasi wasijitukuze nafisi zao" (Zaburi 66:7). "Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote" (Zaburi 103:19).

USIOGOPE

David Wilkerson (1931-2011)

Bwana ana subira sana kwa watoto wake. Kwa kweli anatualika, "Toeni hoja zenu zenye nguvu" (Isaya 41:21), maana yake ni vizuri kuwa na muda wa kuhoji. Tunaweza kupata habari za ghafla na zenye kutisha - kifo cha mpendwa, kutaka talaka ya mwana au binti, uaminifu wa mwenzi. Wakati huo, Mungu anatuma Roho Mtakatifu kutuletea faraja, kupunguza maumivu yetu, na kutuliza mioyo yetu. Bwana wetu anahisi kila maumivu, hofu na wasiwasi ambayo inatupiga.

PESA YA KODI NDANI YA KINYWA CHA SAMAKI!

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu anaweza kurejesha chochote kilichoonekana kilikufa katika maisha yetu kwa neno moja tu. Je! Una matatizo ya kifedha, hauwezi kulipa bili yako? Hivyo vilifika wakati Bwana arikuwa pamoja na wanafunzi wake.

Wakati wa kodi ulipofika, Kristo na wanafunzi wake hawakuwa na pesa kulipa kiasi kinachohitajika. Basi, Bwana alifanyaje kwa kukerebesha hali hiyo? Alimtuma Petro kwenda kuvua samaki. "Nenda baharini, ukatupe ndoano, na uchukue samaki unaokuja kwanza. Na ukifunguwa mdomo wake, utaona chekeli; ichukuwe hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako" (Mathayo17:27).