Body

Swahili Devotionals

JE! TUNA SHAUKU YAKUWONA IMANI YETU INASAFISHWA?

David Wilkerson (1931-2011)

Wapenzi, Mungu anataka watu ambao wanamtegemea kikamilifu. Bwana hakutuokoa ili tuweze kuzunguka kwa kudumu katika wema wake, rehema na utukufu. Alikuwa na kusudi la milele katika kuchagua kila mmoja wetu na kusudi hilo linakwenda zaidi ya baraka, ushirika na ufunuo. Ukweli ni kwamba, Mungu bado anafikia wanadamu waliopotea, kutafuta watu wenye Imani, anaweza kubolesha kama chombo chake kikubwa cha uinjilisti.

ITIKADI KALI, NI OMBI LENYE KUKATIZA

Gary Wilkerson

Katika Mahubiri ya Mlimani (Luka 6:20-22), Yesu anatoa orodha yanao fanya mambo au shughuli ambazo mtu atabarikiwa. Anazungumza juu ya kuwabariki wale ambao ni wanyenyekevu, wale walio masikini katika roho na wale ambao ni wafuasi. Orodha hii imejulikana kama "Furaha ya ajabu." Hata hivyo, furaha ya ajabu hayikujumuisha, "Heri ni wenye kuwa na mashaka, kwa kuwa hawataweza kupooza."

UNYENYEKEVU KABLA YA AHADI

Carter Conlon

Siku ya Pentekoste, Petro alihubiri, "Tubuni, mkabatiziwe kila mmoja  kwa jina lake Yesu Kristo" (Matendo 2:38). Kwa maneno mengine, "Vua mbali njia zako za zamani ya kuishi na majaribio yako yote ya kuwa watakatifu kwa nguvu zako mwenyewe. Vua muonekano wa kuwa Mkristo, na uvae Kristo. Na mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu, maana ahadi ni kwa ajili yenu!"

KWA NINI YESU ALIONGOZWA JANGWANI ILI APITIE MAJARIBIO?

David Wilkerson (1931-2011)

"Kisha Yesu alipandishwa na Roho jangwani, ili ajaribiwe na ibilisi" (Mathayo 4:1). Msitari wa ajabu. Mathayo anasema kwa ujasiri kwamba Roho wa Mungu alimwongoza Kristo katika uzoefu wa jangwa, ambako angelazimika kukabiliwa na majaribu makubwa. Kwa kushangaza zaidi, aya hii inafuata moja kwa moja eneo la utukufu mkubwa wakati Yesu alikuwa amebatizwa tu katika Mto Yordani. Alipotoka nje ya maji, mbinguni ilifunguliwa na Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na akaa juu ya bega lake.

"KAMA MTU MWENYE MAMLAKA"

David Wilkerson (1931-2011)

Baada ya Yesu kutoa Mahubiri kwenye Mlima, wasikilizaji wake waliketi kwa kushangaa. Andiko linasema, "Watu walishangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha" (Mathayo 7:28-29). Neno la Kiyunani kuhusu mamlaka katika aya hii ina maanisha "kwa ustadi, kwa nguvu, kama moja ya udhibiti." Wasikilizaji wa Yesu walikuwa wakisema, kwa kweli, "Mtu huyu anaongea kama anajua anayosema."

WIMBO UNAOFAA, UPANDE USIOFAA

David Wilkerson (1931-2011)

Katika dhambi zote tunazoweza kufanya, kuwa namashaka ni kitu kimoja ambacho kinachukiwa sana na Mungu. Kwa mujibu wa Agano la Kale na Agano Jipya, mashaka yetu huhuzunisha Bwana. Tunaona mfano mkuu wa hii katika Israeli ya kale baada ya Mungu kuwaokoa watu wake kutoka kwa mkono wa Farao.

"Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu, tumetenda maovu, tumefanya mabaya. Baba zetu katika Misri hawakufikiri matendo yako; hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, wakaasi kwenye bahari - bahari bahari ya shamu" (Zaburi 106:6-7).

TUMEITWA KUSHIRIKIANA NA YESU

Jim Cymbala

Je, unajua baba ambaye hazungumzi tena na mwanawe? Labda wakati mmoja walikuwa karibu, lakini maneno makali yaliyosemwa wakati wa hoja amabao hawajawahi kuzungumza tangu. Au labda unajua wanandoa ambao huwasiliana mara kwa mara na hawafurahie mambo ya kila mtu kwa kila upande. Watu hawa wana uhusiano lakini hawana ushirika kati yao.