YESU, CHANZO CHA FURAHA YOTE
Isaya 16:6 inaelezea kwa wazi wazi kile kinachotokea kwa taifa la kiburi ambalo linaanguka chini ya hukumu ya Mungu: "Tumesikia habari za kiburi cha Moabu ... ya majivuno yake na kiburi chake na ghadhabu yake; lakini uongo wake hautanendelea kuwa hivo." Katika Maandiko yote, taifa la Moabu linatumika kama ishara inayowakilisha watu wote wanaojiamini ambao hugeukia nyuma kutoka kwa Mungu na kuanguka chini ya hukumu yake.