Body

Swahili Devotionals

KUTEMBEA UKUPITIA KWA MAMBO YA KIDUNIA UKIWA NA KUSUDI

Carter Conlon

Tunasoma katika kitabu cha Isaya, "Huwapa nguvu wazamiao, humwongezea nguvu asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazamia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka" (Isaya 40:29-30). Kwa maneno mengine, inakuja msimu katika kila maisha yetu wakati tunasikia hatuwezi kuendelea. Tunasikia kama tunakwenda kusambuka na kuwaka, na kusema, kiroho. Vivyo hivyo, sisi sote tunakabiliwa na msimu wakati baridi inapoingia moyoni mwako - labda kwa sababu ya uhuru wa maisha ya kila siku.

AHADI YA NGUVU NDANI YA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alipokuwa akitumia saa zake za mwisho pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Amini amini, nawaambia, mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu " (Yohana 16:23). Kisha akawaambia zaidi, "Hadi sasa hamkuomba kitu chochote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, ili furaha yenu iwe kamili" (16:24).

JE! NINI KINATOKEA WAKATI KUTOKUAMINI KUNAWEKWA NDANI?

David Wilkerson (1931-2011)

"Msifanye mioyo yenu kuwa mingumu kama wakatika wa kukasirisha, siku ya kujaribiwa jangwani, ambapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, na wakona matendo yangu yangu miaka arobaini. Kwa hiyo nilichukizwaa na kizazi hiki, nikasema, "Daima hupotea moyoni mwao, wala hawakuzijua njia zangu." Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, "Hawataingia katika raha yangu" (Waebrania 3:8-11).

SALA LA KUPAMBANA NA MALENGO YA SHETANI

David Wilkerson (1931-2011)

"Muwe na busara, kuweni macho; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka, akitafuta mtu ammezaye" (1 Petro 5:8).

Biblia inatuambia waziwazi kwamba katika siku hizi za mwisho, Kanisa la Yesu Kristo linakabiliwa na ghadhabu ya shetani mwenye hasira. Shetani anajua wakati wake ni mfupi na yeye ni tayari kuharibu watu wa Mungu (angalia Ufunuo 12:12). Shetani huelekeza wapi ghadhabu yake? Anachukua lengo kwa familia pote duniani na lengo lake ni rahisi: kuleta uharibifu na uharibifu kwa kila nyumba iwezekanavyo.

NINI KINACHOKUZUIA?

Gary Wilkerson

"Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorinto; mioyo yetu imekunjuliwa" (2 Wakorintho 6:11). Paulo anazungumza na kanisa linaloingia msimu mpya. Wana historia nzuri na yenye utukufu, lakini pia wamevumilia majaribio na shida.

Kila mtu anayesoma hili ina kitu sawa na kila mtu mwingine: kinachoitwa mwili - kitu ambacho kinakufanya usisogeleye ubora zaidi wa Mungu. Kanisa la Korintho lilijaa kile ambacho Paulo aliita uhai - uasherati, migawanyiko kati yao - lakini Paulo anawahakikishia kuwa moyo wake umefunguka juu yao.

KUPATA BARAKA ZA MUNGU

Jim Cymbala

Moja ya siri muhimu ya kupata baraka za Mungu ni kutoa! Wakati Musa alipokuwa akiwapa maagizo yake ya mwisho ya kuwaaga Waisraeli, alitoa maelekezo maalum juu ya kitu kinachoitwa "fungu la kumi la mwaka watatu." Tofauti na fungu la kumi la kawaida, au asilimia kumi ya sadaka ya kila mwaka, sehemu ya kumi ya miaka ya tatu ilihifadhiwa mambo tofauti.

IKIWA UTAMWITA TU

David Wilkerson (1931-2011)

Katika miaka ya kwanza ya Kanisa, mateso makubwa yalifanyika. Katika kipindi hicho cha kutisha, mtume Yohana alichukuliwa kama mfungwa na kupelekwa Roma kabla ya kutupwa kwenye Kisiwa cha Patmo ili akufe. Patmos ilikuwa eneo ndogo, ambalo lililokuwa pekeyake na kutoishi watu isipokuwa tu wafungwa wengine wachache ambao walikuwa wamekimbilia huko.

Wakati Yohana alipobebwa Patmos, alisalia, akaachwa, akitengwa. Baadaye akaandika, "Nimetupwa Patmos kwa neno la Mungu na kwa ushuhuda wa Yesu Kristo" (angalia Ufunuo 1:9).

WATUMISHI WALIOGUSWA NA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Danieli akashuhudia, "Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu" (Danieli 10:10). Neno la "kuguswa" hapa linamaanisha kushikilia kwa ukali. Danieli alikuwa akisema, "Mungu alipoweka mkono wake juu yangu, inaniweka juu ya uso wangu; kugusa kwake kunanijaza kwa haraka kumtafuta kwa kila kitu kilicho ndani yangu."