WALINDA USALAMA DHIDI YA VIWANJA VYA SHETANI
Katika barua yake kwa kanisa, Yuda anatoa onyo la maana: "Kwa wale walioitwa, waliotakaswa na Mungu Baba, na kuhifadhiwa katika Yesu Kristo: Mwongezewe rehema, amani, na upendo ... Niliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mshindanie Imani waliyokabithiwa watakati mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, watu wasiomcha Mungu, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana Bwana pekee yake Mola Mungu, na Bwana wetu Yesu Kristo" (Yuda 1-4).