Swahili Devotionals | Page 94 | World Challenge

Swahili Devotionals

ABBA, YAANI, BABA

Gary WilkersonOctober 30, 2017

Isaya 6 ina fungu la utukufu sana kuhusu Yesu: "Nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu saana na kuinuliwa sana,na pindo zazazi zikalijaza hekalu” (Isaya 6:1). Kukua sana, maono yangu ya Bwana ndani ya mawazo yangu ni kwamba alikuwa mahali pa mbali, kuondolewa kutoka kwangu, chombo nilichohitaji kushughulikia katika lugha ya Biblia ya Mfalume Yakobo (King James Bible) kama "Wewe" na "Wewe.”

Tena nini Mungu wetu mtakatifu wa juu, anasema juu yetu sisi watu wa chini, watenda dhambi wanaomfuata? Isaya anatuambia hivi: "Maana yeye aliye juu, na aliyetukuka,akaaye milele ; ambaye jina lake ni Mtakatifu; “asema hivi ;nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu ;tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzizfufua roho za wanyenyekevu,na kuifutua mioyo yao waliotubu” (57:15). Ndiyo, Baba yetu ni mtakatifu, mwenye utukufu na sifa - hata hivyo anajinyenyekeza kukaa ndani ya mioyo yetu yenye unyenyekevu, yenye dhambi.

Nadhani kila mtoto kwakawaida anajua tofauti kati ya kupenda dini na kumpenda Yesu. Siku moja wakati binti yangu alipokuwa mdogo, alipekua kati ya ukurasa wa gazeti nililokuwa nikisoma. Nilikuwa nimechoka na nikamfukuza, nikitaka dakika chache tu kupumzika kabla ya kufanya kazi kwenye mahubiri niliyohitaji kwa Jumapili ijayo. Lakini yeye aliendelea kupekua, akisema, "Baba, nataka kukuambia kitu fulani.” Niliendelea kumufukuza mbali, kufikiri saa na kuweka harama kwene dakika za kupumuzika. Haya mbele na nyuma yalisimama wakati mimi hatimaye nikasema, "Asali, unataka kuniambia nini?" Akajibu, "Ninakupenda.”

Alijua tofauti kati ya dini - ukamilifu wangu kama mhubiri - na kumpenda Yesu, ambayo alikuwa ananionyesha. Neno la Mungu linaweka wazi kwamba anataka sisi tumusogelee kama binti yangu alivyonitendea - ita saana "Baba," Abba, ambaye yu karibu saana, si mbali au kupita zaidi ya kutufikia. 

Download PDF

UJUMBE PEKE YAKE HAUTOSHI

Jim CymbalaOctober 28, 2017

Wanafunzi walikuwa na nia ya kuanza kuhubiri lakini Yesu aliwaagiza "Lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu" (Luka 24:29). Yesu alijua vizuri zaidi kuliko wanafunzi, kwamba vifaa vinavyohitajika kwa kazi ilikuwa zaidi ya akili nzuri, talanta ya binadamu, na hata moyo wa kweli. Kwa hiyo walitii agizo la Yesu na walisubiri chumba cha juu, wakiomba na kuimba, pamoja na kumsifu Mungu.

"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyo wajalia kutamka” (Matendo 2: 1-4).

Roho alimwagiwa kama Yesu alivyoahidi. Nini nabii Yoeli alitabiri kilichotokea. "Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu nab inti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto” (Matendo 2:17). Hii ilimaanisha kwamba aina mpya ya uwezo ilipatikana. "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu" (Matendo 1:8). Nguvu hii ya ajabu kutoka mbinguni ilitakiwa duniani ili kujenga ufalme wa Kristo.

Je, wanafunzi hao walikuwa waumini wa kweli wa Yesu waliomngojea Yerusalemu? Ndiyo. Je, Walikuwa na mafundisho sahihi? Ndiyo. Je, wangeweza kwenda na kuhubiri bila Roho Mtakatifu? Nina hakika walitaka hilo, lakini Yesu alijua hawakua tayari. Alijua uwezo wa adui watakaokabiliyana, kukata tamaa, na upinzani. Ikiwa nguvu ya Roho Mtakatifu ilitakiwa basi, Je, kuna kitu chochote kilibadilika hadi siku ya leo? Je, patakuwa kitu kingine isipokuwa nguvu ya Roho kufanya kazi kupitia kwetu na kubomowa kuta za kutokuamini na kuvunja nguvu za tabia ya dhambi tunapoongea kuhusu injili?

Jim Cymbala alianza na Brooklyn Tabernacle akiwa na wanachama wasio zidi ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.

Download PDF

UPENDO WAKE NI BORA KULIKO UHAI

David Wilkerson (1931-2011)October 27, 2017

Hii ndio mojawapo ya mistari inayotajwa zaidi na ya wimbo wote katika Neno la Mungu: "Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu" (Zaburi 63:3). Unaweza kuuliza, "Ina maana gani kwamba fadhili zake ni njema kuliko uhai?"

Ukweli ni kwamba, maisha ni mafupi. Anakuwa alafu kupotea kama majani, ambayo yapo msimu mmoja na kupotea kataki msimu mwengine. Hata hivyo, upendo wa Mungu hudumu milele. Miaka milioni tangu sasa Yesu atakuwa kama huruma na upendo kwetu kama alivyo sasa. Wengine wanaweza kuchukua maisha yako mbali na wewe, lakini hawawezi kuondoa fadhili na upendo wa Mungu.

Fikiria hili kwa muda: Mungu hawapendi kwa sababu ya kushindwa kwako. Ikiwa uko tayari kuacha dhambi yako, unaweza kusamehewa na kurejeshwa kwa wakati huu. Neno la Mungu linatuambia kwamba hakuna chochote kinaweza kuwa kiziwizi kati ya Bwana wetu na sisi - hakuna dhambi, hakuna hatia, na hakuna mawazo ya kukuhukumu. Unaweza kusema, "Maisha yangu ni baraka kwa Bwana, ninaweza kufurahi na kumsifu."Mimi ni safi, huru, kusamehewa, kuonekana kama mwenye haki, kutakaswa, ukombolewa. "

Haijalishi jinsi ni vibaya kwaale walio karibu nasi wamefanya dhambi. Mungu bado anapenda wote. Ndiyo sababu alimtuma Mwanawe. Na tunapaswa kuhubiri hilo kwa ulimwengu!

Daudi akasema, "Sikuficha fadhili zako wala kweli yako katika kusanyiko kubwa" (Zaburi 40:10). Hiyo ndio hamu yake kwa sisi sote.

Una Baba mwenye upendo, mwenye huruma ambaye anajali juu yako. Amevaa kila machozi ambayo umewahi kumwaga. Ameona mahitaji yako yote, anajua mawazo yako yote. Na yeye anakupenda! Ikiwa ungeweza tu kuelewa ni jinsi gani anavyokuwa na huruma kwako - jinsi anasubira, akijali, tayari kukusamehe na kukubariki - hawungeweza kujaza wewe mwenyewe. Ungepiga kelele na kusifu mpaka sauti yote ipoteye kabisa: "fadhili zake ni bora kuliko uhai!”

Download PDF

TUNAHITAJI KUMSHUKURU MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)October 26, 2017

Yona alikuwa nabii ambaye alielewa kikamilifu fadhili za Bwana. Lakini alikuwa mtu ambaye hakuweza kufurahia au kuifaa. Badala yake, Yona akageuza huruma ya Mungu kuwa mzigo kwa ajili yake mwenyewe.

Mungu alikuwa amemwamuru Yona kwenda mji mwovu Ninawi na unabii wake wa uharibifu wa haraka. Unaona, watu wa Ninawi walikuwa maadui wa Israeli. Lakini Yona akakimbia kwa haraka alipoposikia maagizo ya Mungu? Nini kilichochochea uwajibu wake uliokithiri, nikwa sababu alijua upendo wenye huruma wa Bwana. Yona alimwambia Bwana, “Kwamaana nalijuwa ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya" (Yona 4:2).

Kwa maneno mengine: "Mungu, umeniamuru niambie Ninive kama wana siku arobaini kabla ya uharibifu unakuja lakini siwezi kufanya hivyo kwa sababu najua wewe. Unaguswa kwa urahisi. Machozi na toba hulegeza moyo wako na najua nini kitatokea. Iwapo utaona watu wa Ninawi wakalia, utabadili mawazo yako badala ya kutuma hukumu utawachochea mioyo yao - nami nitaishia kuangalia kama mpumbavu!"

Hatimaye, Yona alikwenda Ninive, lakini tu kwa njia ya tumbo la samaki kubwa, ambayo alimutapika kwenye ardhi kavu. Yona alitangaza hukumu ya Mungu kwa Ninive na, kwa hakika, watu walitubu. Dhambi ngumu za watu wa Ninawi ziliwatuma kulia, wakafunga, wakaomboleza na kuvaa magunia, hata kufunika wanyama wao kwa nguo za kuomboleza. Ilikuwa mojawapo ya uwamusho mkubwa zaidi ulioandikwa katika Biblia.

Lakini katikati ya hayo yote, Yona akakasirika. Kwa kweli alisimama kwa sababu Mungu aliwaokoa Ninive badala ya kushangilia kwamba walikuwa waadilifu. Kwa kifupi, Yona hakufurahia upendo wenye huruma wa Mungu.

Wapenzi, kama watu wa Mungu, hatuwezi kufanya makosa sawa. Tunahitaji kumshukuru Mungu kwa nema yenye upendo wa huruma juu yetu, kwa kanisa lake, na kwa taifa letu.

Download PDF

MUNGU HUFURAHIYA WA TOTO WAKE

David Wilkerson (1931-2011)October 25, 2017

Hapa ni silaha yenye nguvu kwa kila mfuasi wa Yesu: Lia! Lia sana kwa moyo wako wote kama Daudi alivyofanya (angalia Zaburi 34:6). Nenda kwa Bwana na ukiri dhambi yako na kujitokezea mbele ya mapenzi yake, ukisema, "Bwana, najua unanipenda na uko tayari kunisamehe, natubu mbele yako hivi sasa."

Kwa wakati huu unakiri, wewe hauna tatizo na Mungu tene. Ni bure kufikiri unaweza kulipa kiasi chochote kwa dhambi yako. Mungu anakupenda sana kiasi kwamba akamtoa Mwanawe, Yesu, ambaye tayari amefanya malipo yote. Msaidizi wako mwenye rehema na upendo ana hamu ya kukusaidia na kukupa: "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Nakama mtu akitenda hdambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki" (1 Yohana 2:1).

Strolling akitembea sambamba pamoja na mjukuu wangu mdogo, Tiffany, akipitia ukuta wa chini wa saruji. Nilimchukua kutoka nyuma ili kumzuia kuanguka, lakini alijaribu kujitoa mikononi mwangu. Hatimaye nirimuachilia aende, naye akaenda zaidi, ingawa bila kujijeruhi mwenyewe. Alipoanguka, sikumuacha mwenyewe, bila shaka. Sikusema, "Angalia ulifanya nini. Wewe sio wangu tena!" Hakuna babu wa upendo ataweza fanya hivyo.

Bwana alinionyeshea kupitia uzoefu huo, "Daudi, unaruhusu upendo huu kwa mtoto huyu. Lakini wakati mwingine huruhusu mimi kukupenda kwa njia ile ile. Unajivunia saana watoto wako, lakini wakati mwingine umeshindwa kuniruhusu kujivunia ndani yako.”

Nikasikia Bwana akisema neno la huruma kwa moyo wangu. Alisema, "Mwanangu, unanibariki, unabariki moyo wangu!" Hakuna mtu aliyewahi kusema kitu bora kwangu katika maisha yangu. Tena najua neno hili ni kweli. Mungu hufurahia watoto wake (Zaburi 147:11).

Download PDF

KUWA TAYARI KUSAMEHE

David Wilkerson (1931-2011)October 24, 2017

Inajulikana vizuri kwamba Mfalme Daudi alianguka katika dhambi mbaya, akafanya uzinzi na kuifunika kwa mauaji. Zaidi ya hayo, tunajua Daudi alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, kwa hiyo lazima alikuwa mwenye huzuni nyingi.

Nabii Nathani akamwambia, “Umeletea jina la Mungu aibu" Daudi angeweza kwenda kwa muda mrefu sana kubeba uzito wa matendo mabaya aliyoifanya na mara moja alikiri na kutubu. Hata kama alipokuwa akilia, Nathani alimhakikishia, "Bwana naye ameiondowa dhambi yako, hutakufa" (2 Samweli 12:13).

Hata hivyo, kusikia kwamba uhakika huo haukutosha Daudi. Unaona, ni kitu kimoja kusamehewa na kuwa kimya kwaupande mwingine kuwa huru na wazi na Bwana. Daudi alijua kwamba msamaha ulikuwa sehemu rahisi. Sasa alitaka kupata haki ya vitu pamoja na Mungu, ili apate kupata furaha yake tena. Kwa hiyo akasema, "Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee" (Zaburi 51:11).

Zaburi 51 imeandikwa wakati Daudi alikumbuka hali ya huruma na uvumilivu wa Bwana. Katika mstari wa ufunguzi anaomba msamaha wa huruma wa Mungu: "Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako, uyafyte makossa yangu."

Daudi alijua tu cha kufanya. Alilalamika! "Masikini huu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa natabu zake zote" (34:6).

"Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao ... walilia, naye Bwana akasikia, akawaponya na taabu zao zote" (Zaburi 34:15 na 17).

Ndugu mtakatifu, ushindi wako juu ya vita vyote ni kujifunza kuwa na imani hii: Bila kujali jinsi ulivyoanguka sana, unamtumikia Bwana aliye tayari kusamehe. Hakika, ana hamu ya kukuponya. Yeye ana upendo zaidi kwako kuliko vile unavyohitaji.

Download PDF

KUCHUKIA DINI

Gary WilkersonOctober 23, 2017

Kwa sababu nataka watu wote ulimwenguni kujua ukweli wa Yesu, ninatumia muda mwingi wa kutembea duniani kote katika huduma. Na kisha nitakaporudi nyumbani, ninaomba kwamba kila Mkristo atamjua Yesu pia!

Natumaini umepata utani - lakini unahitaji kujua kama nina nusu tu ya kutania. Maisha yetu kama wafuasi wa Kristo sio juu ya dini inayojulikana, lakini juu ya Mtu anayeweza kujulikana, Yesu. Kuna tofauti kubwa.

Biblia inatuambia mambo matatu yanayotupinga sisi katika kutembea na Kristo: dunia, mwili wetu na shetani (tazama Waefeso 6:12). Nimejiuliza, "Kwa nini dini sio ndani ya orodha hiyo wakati inapinga uhusiano wetu na Yesu, pia?" Kisha nikaona dini ni katika yote matatu!

Wakati ninapotumia neno "dini,” nina maanisha mambo ya wudini. Hili ni wazo kwamba tunaweka dini - imani na mazoea yetu ya kitheolojia - katikati ya maisha yetu badala ya Mungu mwenye upendo. Ni ndani ya Yesu kwamba tunaishi, kupumua na kuwa na utu, sio mfumo wa imani au kazi.

Unapoiangalia kwa njia hiyo, dini inakuwa mfano wa mwili wetu, maana ya tabia yetu ya dhambi. Mwili wetu hutumia dini kama musitali wambele ili kupinga kutubu na hutufanya kujisikia vizuri kuhusu sisi wenyewe. Mjomba wangu Don Wilkerson anaita hii “kusonga mbele." Kurudi nyuma ni wakati watu wanapoanguka mbali na Yesu kwa kugeukia dhambi kubwa. Kusonga mbele ni kuanguka kwa upande mwingine, kugeuka kuelekea dini na mbali na kuwa mbali na Yesu.

Hebu aca tukumbane nalo, kwasababu dini inaweza kuwa na urahisi zaidi kuliko kujazwa na upendo wa Yesu, kwa sababu ya kuongozwa na upendo wake kunaweza kutufanya tuonekane kuwa watu wamechanganyikiwa kidogo kwa watu wa dunia.

Tafadhali usinielewe vibaya wakati ninasema tunapaswa kuchukia dini. Ninachosema ni kwamba tutachukia mambo ambayo yanaongoza kifo cha kiroho badala ya maisha ya kweli katika Kristo. Kuchukia dini haimaanishi kupenda mwili wako; inamaanisha kumpenda Yesu zaidi.

Download PDF

GOTT HAT BEREITS GESPROCHEN

Carter ConlonOctober 21, 2017

Kuna sababu nyingi kwa Mungu kuwa kimya, lakini nitaenda kugusa juu ya kitu ambacho yeye hivi karibuni ameweka ndani ya moyo wangu. Wakati mwingine Mungu anaweza kuwa kimya tu, kwa sababu tayari arisha sema nawe! Ikiwa unafikiri juu yake, unawezaje kumshtaki Mungu wa kuwa kimya wakati amekuachia barua sitini na sita, maelfu ya mistari? Hakuna haja ya kurudiaemwo mwenyewe tena. Je, hufurahi kwamba kitabu cha Mwanzo hasema, "Mungu akasema, iwe nuru. Ikawa nuru”?

Ikiwa wewe na mimi tulikuwa huko siku hiyo ya kwanza ambapo Mungu alisema, "Iwe nuru," tungekuwa tumecheza na kufurahi ya kutoka saa 6 asubuhi hadi saa 6 jioni.

Lakini ghafla, inapoanza kuwa giza, tunaanza hofu. "Loo, hapana, nilitambua kwamba hakutaka dumu! Nilijua mwanga unakwenda mbali. Labda tumefanya kitu kibaya. Labda hatukusoma Neno la kutosha.”

Nuru inaondoka, na tunatumia masaa kumi na mbili ajayo kwa huzuni - mpaka mwanga utakaporudia tena, na tunatambua kwamba wakati Mungu alisema, "Iiwe nuru," hakumanisha kwamba hapatakuwa na usiku; kwamba hakutakuwa na msimu ambapo hatuwezi kuona. Hakumanisha kwamba tutaweza kuelewa kila kitu kinachoendelea katika ulimwengu wa mbinguni. Hata hivyo, mwanga daima huonekana tena, na tunaona kwamba kile Mungu alichosema kinaendelea kutimizwa bila yeye kusema tena.

Sababu moja ambayo Mungu anaweza kuwa kimya ni wakati uliowekwa wa Neno lake ili litimizwe. Mfano mmoja wa hili katika Biblia ni Joseph, ambaye alipewa ahadi ya ajabu kwamba angetawala siku moja. Alitaka kuwa mtu wa njia ambayo utoaji mkubwa utafunguliwa. Hata hivyo, kulikuwa na muda uliowekwa wa utimilifu wa ahadi na alitakiwa kufuata mpango wa Mungu.

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.

Download PDF

"WALIMULILIA SAANA BWANA"

David Wilkerson (1931-2011)October 20, 2017

Biblia inaahidi kwamba inawezekana kuelewa upendo wa Bwana. Je, ni ufunguo gani? Mfalme Daudi akasema, "Aliye na hekima ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za Bwana" (Zaburi 107:43).

Daudi alipata ufunuo wa kushangaza kwa neema ya Mungu, na moyo wa kusamehe. Na aligundua tu kwa kuangalia rekodi ya Mungu ya zamani ya kushughulika na watoto wake wapendwa. Daudi anaripoti kwa hii njia:

"Waliona njaa, waliona na kiu, nafusi yao ilikua ikizimia ndani yao, wakamlilia Bwana katika dhiki zao, akawaponya nashida zao, akawaongoza kawa njia ya kunyoka…na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, na maajabu yake kwa wanadamu!" (Zaburi 107:5-8).

Wakati wana wa Israeli walipotea mbali na Bwana, wakawa na njaa, wakaona kiu na kupotea kwa sababu ya dhambi. Lakini basi wakaliliia Bwana, na nini kilichotokea? "Maana hushibisha nafsi yenye shauku, na nafsi yenye njaa huijaza mema" (107:9).

Hata hivyo waliasi na kurudi nyuma, wakianguka chini kabisa. Tena tunasoma: "Wakamlilia Bwana katika dhiki zao ... hulituma neno lake, huwaponya" (107:19-20).

Hatimaye, watu wa Mungu walikuja tena na uwezo wao wa mwisho wa kufikili. Dhoruba ilio haribu na nafsi zao ziliyayushwa na shida: "Kisha wanamlilia Bwana katika taabu yao, na anawaondoa katika taabu zao, huwafungua dhoruba, na mawimbi yake bado" (107:28-29).

Daudi alijibu kwa ufunuo huu, "Angalia jinsi moyo wa Mungu unavyogeuka kwa urahisi.Hakika, kwa haraka anaitikia kilio cha watoto wake ... Hakuna huruma kwa huruma zake."

Mpendwa, huhitaji kuendelea na uchungu na hatia. Badala yake, nenda kwa Bwana, kilio na kumkiri kwake. Yeye ni Baba mwenye huruma ambaye huguswa na kila kilio chako.

Download PDF

SAHAU YALIOPITA

David Wilkerson (1931-2011)October 19, 2017

Msingi wa ushindi wote juu ya dhambi ni ufahamu kwamba Mungu ni mwenye huruma na mwenye kujaa wema na upendo.

"Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifu na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi" (Yeremia 9:23-24).

Ikiwa umetembea na Bwana kwa muda wowote, labda umewahimiza wengine kuwa Mungu ni mwenye huruma na kusamehe. Sasa, napenda kukuuliza: Unaposhindwa kwa Bwana, je, ni jambo tofauti la gafla ? Je, Unajikuta ukifanya kazi kupitia hisia za kuwa mwenye hatia na aibu?

Unaweza kusema, "Je, Hatupaswi kuwa na uzoefu huo wakati tunapofanya dhambi?" Hakika, hisia hizo ni matokeo ya asili ya dhambi. Lakini kama watoto wa Mungu hatupaswi kuendelea kwa siku na wiki kufikiri kwamba Baba yetu anadharauliwa kwetu. Kwa sababu ya utoaji wa Kristo msalabani, hatia yote na hukumu inaweza kuinuliwa haraka.

Inaendelea, hata baada ya kutubu, tunaweza kuhisi kwamba tunapaswa kushindwa kushindwa kwa Bwana. Kama Mwana Mpotevu, tunaweza kuwa na Baba anatukumbatia, na kuweka pete kwenye kidole chetu na vazi kwene mgongo wetu. Anatuambia sisi kusahau yaliopita na kufurahia sikukuu aliotayarisha kwa ajili yetu.

Lakini ndani tunaasi, "Sistahili! Nimenda dhambi dhidi ya Bwana, ni lazima nimwoneshe kwamba na omba musamahani."

Wakristo wengi wanaona kama nirahisi kuamini kwamba Mungu aliwasamehe dhambi kubwa za Israeli. Hatuna shida kukubali kwamba alisamehe Ninawi katika Agano la Kale na mwizi aliyekufa katika Agano Jipya. Lakini, isiyo ya kawaida, ni vigumu kwetu kuelewa kwamba wakati tunamgeukia kwa kutubu kwa haraka na kwa upendo hutukubali sisi kama wenye hajawahi kutenda dhambi.

Download PDF