JE, NINAJIFANANISHA NA ASILI YA KRISTO?

David Wilkerson (1931-2011)

"Kuweni na nia ndani yenu ambayo pia ilikuwa ndani ya Kristo Yesu" (Wafilipi 2:5).

"Lakini sisi tunayo akili ya Kristo" (1 Wakorintho 2:16).

Ushauri huu kutoka kwa mtume Paulo unawaambia watu wa Mungu, "Hebu acha mawazo yaliyo ndani ya Kristo - mawazo ya Yesu - awe mawazo yako pia. Kufukili kwake ni kule sisi sote tunakotaka."

NANI ANAYEFANYA MAAGIZO KATIKA MAISHA YAKO?

David Wilkerson (1931-2011)

"Tukiishi kwa roho, na tuenene kwa Roho" (Wagalatia 5:25). Mtume Paulo anatupa maagizo haya rahisi sana kwa maneno wazi, "Ikiwa Roho Mtakatifu anaishi ndani yenu, aca awe na udhibiti kamili wa maisha yako."

Sisi sote tunaongozwa na Roho. Alitumwa kuwa muda wetu wa daima, asio kuwa na makosa, na anaishi katika wote wanaokiri Kristo kama Bwana na Mwokozi. Wakristo wengi hawana shida kukubali kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza kwa Yesu, na hatuna shida kuamini kwamba Roho anaendelea kufanya kazi ndani yetu wakati wote.

NJAA ILIYOLETWA NA KUTOSAMEHE

David Wilkerson (1931-2011)

Msamaha si tu hatua ya wakati mmoja lakini ni njia ya maisha, maana ya kutuleta katika kila baraka ndani ya Kristo. "Nawaambieni, wapendeni maadui zenu, wabariki wale wanaowauzi, fanyeni mema kwa wale wanaowachukia, nawaombeeni wale wanaowatumia kwa udanganyifu na kuwatesa, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni" (Mathayo 5:44-45).

MOYO WA MCHUNGAJI

Gary Wilkerson

Maisha yangu mengi nilikuwa na dhana iliyopotoka sana ya wachungaji. Wakati niliposikia hadithi za Biblia kuhusu Daudi mchungaji, nilimchola akiketi juu ya mwamba, akicheza ngoma yake na kuangalia kondoo wakati wakimzunguka wakiwa kimya. Lakini nilikuwa na picha tofauti kabisa ya wachungaji nilipowaona kwa wenyewe huko Romania miaka michache iliyopita. Wanaume wanaofanya kazi kwa bidii walikuwa wakitafuta daima maeneo yenye kuwa na majani safi ya kulisha na maji ya kunywesha.

UNATAKA KUTUMIWA NA MUNGU?​

Carter Conlon

Hizi ni nyakati ambapo mtu, au labda watu wengi, wanafahamu nia ya Mungu ya kurejesha na kuponya. Wanaelewa nia yake ya kutuchukua, si kwa nguvu zetu, bali katika udhaifu wetu. Baada ya yote, Maandiko haituambie kuja kwenye kiti cha enzi cha Mungu wakati tunapokuwa na nguvu; badala, tunakuja wakati sisi ni dhaifu. "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" (Waebrania 4:16).

ONYO DHIDI YA INJILI LOJOLOJO

David Wilkerson (1931-2011)

Nia moja kubwa ya Baba yetu wa mbinguni ni kwamba hakuna " hata injili nyingine" itaweza kutuweka mbali na msalaba wa Yesu Kristo. Wakristo wengi wamepoteza imani yao kwa sababu walipewa neno la kupendeza miaka mingi iliyopita, labda kitu kama hiki: "Utakuwa na huduma kubwa na kushinda maelfu ya roho kwa Bwana," na hakuna hata neno moja liliotimiza hayo. Sasa kondoo hao wamevunjika kabisa, imani yao imejengwa kwenye dundu la majivu.

KUTOJUA NGUVU ZA ROHO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mara nyingi tunaweza kuwa na kitu muhimu bila kutambua kikamilifu thamani yake au umuhimu wake. Hadithi inayosemwa ya mkulima aliiolima shamba lake ndogo kipindi cha maisha yake yote, akitengeneza aridhi yenye majiwe mwaka baada ya mwaka. Wakati wa kifo chake, shamba lilipitishwa kwa mwanawe ambaye aliendelea kulilima - lakini mtoto huyo aligunduwa  kusanyiko la dhahabu iliyo kwenye udongo. Chamba lilikuwa limejaa dhahabu na mara moja akawa mtu tajiri. Hata hivyo utajiri ulikuwa umepotea wakati wa baba yake, ingawa ilikuwa vigumu yakuwa kwenye ardhi maisha yake yote.

FUNZA SIKIO LAKO KUSIKIA SAUTI YA KRISTO

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu bado anaongea na watu wake leo. Na anasema wazi kama alivyofanya katika Agano la Kale, au kwa mitume, au kwa kanisa la kwanza. Hata hivyo tunapaswa kutambua jambo moja: Mungu huchagua kusema tu kwa wale ambao wana masikio ya kusikia.

Marko anatuambia Kristo "aliwafundisha mambo mengi kwa mifano" (Marko 4:2). Katika kifungu hiki, Yesu anasema mfano wa mtu anayepanda mbegu katika shamba. Hata hivyo alipomaliza habari hiyo, umati wa watu ulikuwa unafadhaika na ukajiuliza, "Ni nani huyu mkulima anayeelezea? Na mbegu inawakilisha nini?"

KAZI YA KWANZA YA ROHO MTAKATIFU

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Isaya anatabiri kinachotokea wakati Roho Mtakatifu anashukia watu. "Roho humwagwa juu yetu kutoka  juu, na jangwa kugeuka shamba lenye kuzaa, na shamba lenye kuzaa linahesabiwa kama msitu" (Isaya 32:15). Anasema, "Wakati Roho Mtakatifu atakapokuja, hapo zamani jangwa liliokuwa tasa litageuka shamba la mavuno. Kipande kilichokufa cha ardhi ghafla kinatowa matunda, na shamba hilo la matunda litakua ndani ya msitu; utakuwa na uwezo wa kuchukua vipandikizi kutoka mwaka huu wa misitu baada ya mwaka na kujenga juu ya matunda yako daima."