UCHUNGUZI WANDANI KUTOKA KWA UVUMILIVU WA YOBU
Mjadala wowote juu ya mateso na majaribio lazima uanze na mwamini mwenye kukata tamaa wakati wote - mtumishi mwenye haki, mwaminifu, mwenye kuogopa Mungu, kujitolea kwa sala na ibada. Hata hivyo, wakati huzuni na shida zilipokuwa zimeharibisha maisha yake, huyo mtu alianza kunungunika sana kuhusu Mungu wakati wa mateso yake. "Kama ningemwita naye akaniitikia; hata hivyo singeamini kuwa amesikiya sauti yangu. Yeye anipondaye kwa dhoruba, na kuziongeza jeraha zangu pasipokuwa na sababu" (Yobu 9:16-17).